Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, September 18, 2012

NISHA: AIOMBA BASATA IMCHUKULIE HATUA KALI ZA KINIDHAMU ‘AUNTY EZEKIEL’”…!

WAKATI wadau wa filamu na kazi za wasanii wakimtolea macho Aunty Ezekiel, baada ya picha zake za nusu uchi kusambaa huku zikidaiwa zinavunja maandali ya kitanzania, msanii Salma Jabu ‘Nisha’, amezitolea uvivu picha hizo na kudai kuwa endapo angekuwa na madaraka juu ya BASATA basi angechukua hatua za kumfungia haraka msanii huyo kwa muda.

“Ingekuwawa mimi nipo kwenye uongozi wa juu ya BASATA ningetoa mfano mkubwa ili wasanii wengine wasifanye upuuzi kama huu, unajua kuna watu wakiona wapo kimya wanatafuta visababu vya kijinga ili tu watu wamzungumzie lakini si kwa ishu hii kwani hapa anajiumiza mwenyewe,”
alisema.

Hata aliongeza tabia kama hizi zikiendelea kwa wasanii basi tasnia nzima ya filamu itaendelea kuchukuliwa ni ya wahuni,  na heshima itapungua sana  hata kama wengine wakiwa na si wavunjaji wa maandali ya kitanzania.


Alisema kuwa yapo mambo ambayo msanii anaweza kuyafanya jukwaani mbele ya mashabiki, lakini si kuvua nguo hadharani na kuacha mwili wako ukiwa hauna kitu, kwani ni kitu ambacho kinaleta picha chafu kwa watanzania na hata wadau wengine wanaoishi nje.

No comments:

Post a Comment