Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, September 24, 2012

WATU 83 WAPOTEZA MAISHA KWA AJALI ZA BARABARANI MKOANI SINGIDA KATIKA KIPINDI CHA JANUARI HADI AGOSTI...!

Maandamano ya sherehe ya kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama mkoani Singida.
Mkuu wa wilaya yya Singida Mwalimu Queen Mlozi akikopea maandamano ya magari kwenye sherehe za maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa Singida yaliyofanyika kimkoa kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Na. Nathaniel Limu. 
Mkoa  wa Singida  unakusudia kuendesha zoezi maalumu la ukaguzi wa magari na pikipiki,  ili kuwabaini watu wanaong’oa alama za usalama barabarani na  kuzifunga  kwenye vyombo vyao.
Mkuu wa wilaya ya  Singida Mwalimu Queen Mlozi ametangaza  kiama hicho kwa wahalifu hao wakati akizungumza kwenye  kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani kimkoa yaliyofanyika kwenye uwanja wa namfua mjini Singida.
Amesema pamoja na  uzembe wa madereva, mwendo kasi, ulevi na elimu duni ya usalama barabarani, sababu  nyingine  ya ajali nyingi kutokea ni kutokuwepo kwa alama muhimu za usalama barabarani.
Mlozi amesema  uchunguzi unaonesha wazi  kuwa nyingi ya alama hizo ikiwemo  viakisi  mwanga hung’olewa  na kufungwa kwenye magari na  pikipiki  za watu  binafsi.
Takwimu zinaonesha  kuwa katika kipindi cha  Januari  hadi  Agosti mwaka huu  jumla ya watu 83 wamekufa  na wengine 192 kujeruhiwa  kutokana na ajali 158 mkoani Singida. 

Chanzo: Mo blog

No comments:

Post a Comment