Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, October 4, 2012

AJALI YA GARI KUGONGA MAGARI MATATU NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI...!

JESHI la polisi mkoani Mbeya limesema kuwa ajali iliyokea Tarehe 2.10.2012 huko Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani humo ilitokea majira ya SAA  13:30HRS  HUKO  MLIMA  MBALIZI  BARABARA  KUU  YA  MBEYA/TUNDUMA.
GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI   T. 911 BUV LIKIWA NA TAILER   NO.  T.  814   BTC   AINA  YA  SCANIA  TANKER  ILIYOKUWA  IKIENDESHWA  NA  DEREVA  ASIYEFAHAMIKA  AKIWA    ANATEREMSHA   MLIMA  MBALIZI  ALIGONGANA   USO  KWA  USO  NA    GARI  NAMBA  T.  887  AHT  TOYOTA  HIACE    ILIYOKUWA  IKIENDESHWA  NA  DEREVA  EMMANUEL  S/O  PWELE  AKIWA  ANAPANDISHA  MLIMA  MBALIZI  NA   LORRY  HILO  KUPOTEZA  MWELEKEO  NA   KUGONGA  MAGARI   MENGINE   MAWILI   AMBAYO  NI  GARI  T.  299  BCE/T 322  AWH  SCANIA  LORRY  ILIYOKUWA  IKIENDESHWA  NA  DEREVA  ASIFIWE  S/O  MSANGA,  KYUSA,  MIAKA  34  NA     GARI  T.  671   AWM  FORD  RANGER  D/CABIN  ILIYOKUWA  IKIENDESHWA  NA  RAJAB  S/O  SUDI,  MIAKA  38  MNYAMWEZI  WA  ILOMBA  MBEYA NA  KUSABABISHA  VIFO  VYA  WA  WATU  10  PAPO HAPO.
 KATI  YAO  SITA  {6}  NI  WANAUME  NA  WANNE  {4}  WANAWAKE NA MAJERUHI MMOJA KATI YA 22 WALIOJERUHIWA ALIFARIKI USIKU WA KUAMKIA LEO NA KUFANYA JUMLA YA WALIOKUFA KUFIKIA 11 AMBAYE AMETAMBULIWA NA JAMAA ZAKE NI SANDE  S/O  NJOLE,  MNYAKYUSA,  MIAKA  26,  MKAZI  WA  MBALIZI PIA MAITI MBILI KATI YA 11 ZILIZOHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA ZIMETAMBULIWA NAZO NI:- {1} G. 4360  PC.  SAMSON,  KYUSA,  ASKARI  POLISI  WA  KITUO  CHA  MBALIZI  MBEYA ,  {2} KABASA  S/O  JUSTINE,  MWANAFUNZI  CHUO  KIKUU  CHA  TEOFILI  KISANJI .
 MAJERUHI   22  KATI  YAO 08 WAMELAZWA  KATIKA  HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA, MAJERUHI SITA WALITIBIWA NA KURUHUSIWA KURUDI NYUMBANI AMBAO NI [1] LUSOLINA  D/O  MBILINYI,  MIAKA 38,  MKIINGA  MKAZI  WA MWAMBENE  [2] SHADRACK  S/O  BALENS,  MIAKA 20,  MNYAKYUSA,  MKAZI WA MBALIZI [3] FRANCO S/O RAPHAEL,  MIAKA 38,  MFANYABIASHARA,  MKAZI  WA  MBALIZI [4] DAVID  S/O  SHUNGO,  MIAKA  24,  MFANYABIASHARA  MKAZI  WA  MBALIZI  [5] AGNES  D/O  MSOYELA,  MIAKA  34,  MKULIMA,  MHEHE,  MKAZI  WA  ILEMBO [6] GWAMAKA  S/O   KAMWELA,  MIAKA  25,  MNDALI  MKAZI  WA  MBALIZI NA SABA {7}  WAMELAZWA  KATIKA  HOSPITALI  TEULE   YA  IFISI  MBALIZI .
 IDADI YA MAJERUHI WALIOLAZWA HOSPITALI YA RUFAA NI 08 AMBAO NI:-   [1] EMMANUEL  S/O  PWEZE,  MIAKA  30,  MNDALI  MKAZI  WA  MBALIZI [2] JOYCE  D/O  SHABAN,  MIAKA  7,  MKAZI  WA  MBALIZI [3] MARTHA D/O  RICHARD  SEME,  MIAKA 6,  MKAZI  WA  MBALIZI [4] ALIKO  S/O  ANYELWISYWE  MWAMABISI,  MNYAKYUSA,  MIAKA  2,  KONDAKTA  WA  HIACE    [5] NEEMA  D/O  SANGA,  MIAKA  19,  MKULIMA,  MKAZI  WA  UYOLE  MIZANI  [6] WINIFRIDA  D/O  GEORGE  KADEZEMA,  MIAKA  34,  MNYAMWEZI  MKAZI  WA  MTAKUJA  MBALIZI [7] SISTA  D/O  FUMBO,  MKINGA,    MIAKA  6,   MKAZI  WA  MBALIZI [8] MTU  MMOJA  MWANAMKE/BINTI    HALI  YAKE  NI   MBAYA HAJITAMBUI.
WALIOKUWA WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI   MBALIZI NI:- [1] MHE.  DR.  MARY  D/O   MWANJELWA  {MB}  VITI  MAALUMU  KUPITIA  CHAMA  CHA  MAPINDUZI  {CCM},  MIAKA  47,  MKAZI  WA  BLOCK  “T”    MBEYA  [2] HERMAN  S/O  MATHIAS,  MIAKA  21,  MKULIMA  MKAZI  WA  MLIMA  RELI  MBALIZI [3] EVANCE  S/O  MATHIAS,  MIAKA  23,  MCHAGA,  MKAZI  WA  BLOCK   “T” [4] EMMANUEL  S/O  MGANA,  MIAKA  40,  MBENA  MWANAFUNZI  CHUO  CHA  TEKU  MBEYA   MKAZI  WA  ILOMBA [5] WILLIAM  S/O  JOHN,  MIAKA  28,  MSAFWA,  MWANAFUNZI  WA  CHUO  CHA  TEKU  MBEYA,  MKAZI  WA  BLOCK  “T” [6] RAJABU  S/O  SUDI,  MIAKA  38,  DEREVA   WA  GARI  NO.
  T.671 AWM GARI LA MHE.  MBUNGE, MKAZI  WA  ILOMBA [7] MTU  MOJA  MWANAUME  AMBAYE  BADO  HAJAFAHAMIKA  JINA  HALI  YAKE  NI  MBAYA  HAJITAMBUI . CHANZO CHA AJALI HIYO NI HITILAFU KATIKA MFUMO WA BREKI WA GARI NO. T.911 BUV/T.814 BTC AINA YA SCANIA TANKER.G DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO.
JITIHADA ZA KUMKAMATA ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA SALAMU ZA POLE KWA NDUGU/JAMAA NA MARAFIKI WA MAREHEMU PAMOJA NA MAJERUHI WA AJALI HIYO AIDHA ANATOA RAI KWA MADEREVA WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI NA KUJALI USALAMA KWA KUYAFANYIA UCHUNGUZI NA MATENGENEZO YA MARA KWA MARA MAGARI YAO ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA, VILEVILE ANAMTAKA DEREVA HUYO KUJISALIMISHA MARA MOJA.
 [ DIWANI ATHUMANI – ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment