Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, October 24, 2012

HAYA HAPA NDIO MASHTAKA YANAYOMKABILI LORD EYES...!

Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Charles Kenyela amethibitisha jeshi lake kumshikilia msanii Lord Eyes ambae toka weekend iliyopita taarifa zake zimesambaa baada ya kushutumiwa kuhusika na wizi wa vifaa mbalimbali kwenye gari la mwimbaji Ommy Dimpoz.

Namkariri Charles Kenyela akisema “ni kweli Isaac Waziri Maputo mwenye umri wa miaka 28 alikamatwa tarehe 20 mwezi wa kumi usiku maeneo ya Kinondoni, kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu ni kutokana na taarifa tulizozipata kupitia kwa binti mmoja aitwae Kurushinde Hillary (22) mwenye asili ya kiburushi lakini mkazi wa Mwananyamala kwa Makoma Dar es salaam, alikamatwa siku hiyo hiyo kabla ya Lord Eyes” “Alikamatwa kuhusiana na matukio ya wizi kwenye magari yani kuna mtindo ambao umeibuka ambapo ukipaki gari yako gari nyingine ya wezi inakuja inapaki jirani na gari yako ambapo kwa muda mfupi wanafanya utundu wao wanaoujua, wanafungua gari na kuiba mali iliyoko ndani, mara baada ya huyu binti kukamatwa katika kuhojiwa mtandao wake anaoshirikiana nao alimtaja mtuhumiwa Isaac Waziri Maputo (Lord Eyes)” – Kamanda Kenyela Kwenye sentensi nyingine Kamanda Kenyela amesema “watu wengi wamelalamika kuibiwa laptop zao, mabegi, mifuko na hata silaha kwa maana mtu anakua anajiamini anaacha kwenye gari akiamini kwamba ameshalock lakini watu hawa na mtandao wao wamekua ni hatari kiasi kwamba wameliza watu wengi” “Watuhumiwa hawa wawili Kurushinde na Lord Eyes tunawashikilia kwa tuhuma zipatazo 30, yani matukio mbalimbali 30 pengine yanaweza yakaongezeka ambayo yameripotiwa kutokea katika maeneo mbalimbali kama vile Mlimani City, Kijitonyama, ufukwe wa bahari kama Coco beach, kwenye kumbi mbalimbali za starehe na pia kwenye maeneo ambayo kunakua na harusi, sehemu ambazo kunakua na magari mengi watu hawa ndio huwa wanaitumia hiyo nafasi kufanya uhalifu, tunawashikilia kwa makosa ya wizi”

No comments:

Post a Comment