WANANCHI waishio maeneo ya mipakani katika wilaya za Rombo na Moshi vijijini wameshukuru kiwanda cha sukari cha TPC kwa kuvunja mkataba wake na KNCU wa kusambaza sukari kwa madai ya kuwa na uhakika wa upatikanaji wa bidhaa hiyo.
Wakizungumza na chanzo chetu kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi hao walisema kuwa kitecho cha TPC kuvunja mkataba huo ni ahueni kwa wananchi walio wengi kwani wana uhakika wa kupata sukari.
Bwana Elienengo Ngowi ni mkazi wa kata ya Mwika kusini wilaya ya Moshi vijijini alisema kwa kipindi kirefu wamekuwa na ukata mkubwa wa sukari huku ikiuzwa kwa bei kubwa tena ya ulanguzi tofauti na maelekezo ya serikali.

"Wakati KNCU wakisambaza sukari iliadimika huku kwetu tulikuwa tunakwenda Moshi mjini kununua sukari hivyo kuvunjika kwa mkaataba huo ni ahueni kwetu sisi tunaoishi huku vijijini”alisema Ngowi
Bi Redegunda Tarimo mkazi wa kata ya Nanjarareha Rombo alisema kuwa KNCU isingeweza kusambaza sukari kama ilivyokuwa imeomba kwani ilishindwa kusimamia maduka ya ushirika na hatimaye yakafa.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari juzi mwenyekiti wa bodi ya KNCU aliitaka serikali kupitia wizara ya kilimo chakula na ushirika kuingilia kati sakata hilo ili iweze kurudishiwa kibali cha kusambaza
sukari hiyo kama ilivyokuwa hapo awali.
Kwa upande wake afisa mtendaji mkuu wa utawala wa kampuni ya TPC bwana Jaffary Ally akizungumzia juu ya kusitishwa mkataba baina ya kampuni yake na KNCU kuhusiana na usambazji wa sukari alisema KNCU haikudhi masharti yalioainishwa katika mkataba husika na kuongeza kuwa utendaji wa KNCU haukukidhi viwango vya mkataba husika kifungu cha tisa.
“ Hawa ndugu zetu wa KNCU hawakukidhi viwango na siku zote wamekuwa wakisambaza sukari chini ya kiwango tulichokubaliana na tuliwaita na kuwaeleza bayana kuhusiana na hili kabla ya kuvunja mkataba nao.
Nashangaa kusikia eti wameandika barua wizara ya kilimo wakikata rufaa kuhusiana na hili. Wizara ya kilimo ina uhusiano gani na mkataba husika?”alisema Bw ally.
No comments:
Post a Comment