Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, October 1, 2012

HII HAPA MELI MPYA YA ABIRIA INAYOMILIKIWA NA AZAM...!

Meli ya Azam Marine inayoitwa Azam SeaLink 1 ikiwasili katika bandari ya Visawani  Zanzibar kwa mara kwanza.
Baadhi ya wakazi wa Zanzibar wakipiga picha Meli hiyo iliyowasili Visiwani Zanzibar leo.
Mzee Said Bakheresa (mwenye nguo nyeusi) akikagua mazingira ya Meli hiyo baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar leo.
Sehemu ya Parking yenye uwezo wa kuingiza magari 200.
Muonekano wa ndani wa Lounge ya kumpzikia wasafiri.
Muonekano wa nje. (Picha na Omar Said wa Kampuni ya Bakheresa).

 Meli mpya ya abiria inayomilikiwa na Azam Marine yatia nanga rasmi katika bandari ya Zanzibar. Meli hiyo imetokea Ugiriki na itaaza kazi
baada ya kumaliza taratibu zote za Kisheria za Baharini, kukaguliwa na taasisi husika, na kupata leseni ya kusafirisha abiria na mizigo. Meli hiyo ina uwezo wa kuchukua abiria
1500, mizigo, na magari 270 kwa wakati mmoja. Meli hiyo itafanya safari kati ya Unguja, Pemba na Dar-es-Salaam hivi karibuni ili kuondoa tatizo la usafiri wa maji kati ya visiwa vya Pemba na Unguja ambako kuna tatizo la usafiri tangu kutokea kwa ajali ya MV Spice Islander, na baadhi ya meli kufutiwa leseni za kusafirisha abilia kutokana na meli hizo kutokuwa na hali ya kuridhisha ya kusafirisha watu. Wananchi wamefarijika kuona
tatizo la Usafiri kati ya Unguja na Pemba limepata ufumbuzi baada ya kuona meli hiyo
katika bandari ya Zanzibar na kutumaini kuwa huduma yake itakuwa nzuri na ya
kuridhisha. Wananchi hao pia wamewataka wafanyabiashara kupunguza nauli ili kila
mwananchi aweze kumudu huduma hiyo na wasiwe katika biashara zaidi kuliko kutoa
huduma kwa wananchi wa hali ya chini ambao hutegemea usafiri huo. Meneja wa Azam Marine, Hussein M Said amesema meli yao itakuwa katika kutoa huduma zaidi kuliko biashara ili kuona kila Mwananchi anafaidika na huduma zao, na wataweka nauli za bei nafuu kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment