KATIBU tawala wa mkoa wa Pwani Benadetha Swai amesema kuwa jamii inatakiwa kushirikiana vyema na waandishi wa habari pindi wawapo kazini kwaajili ya kuetekeleza majukumu yao na kuwataka waandishi wa habari kutambua kuwa kazi yao siyo kumchimba mtu bali ni kufanya uchunguzi wa mambo yanayoendelea kwa ajili ya kuiletea jamii maendeleo.
Amesema hayo leo katika mkutano wa wanahabari na wadau wa habari mkoani Pwani ‘Coast Region Press Club’ katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa Pwani ambao alisema tasnia ya habari ni muhimu kwasababu imekuwa ikifanya kazi hata katika mazingira magumu na wakati mwingine kuhatarisha maisha yao kwa maendeleo ya taifa.
Pia amesema ukosefu wa vitendea kazi, mazingira hatarishi kazini, maslahi duni kwa waandishi, teknolojia kuongezeka, kuvamiwa na kushushwa hadhi, tasini hiyo kuvamiwa na watu wasiyokuwa na taaluma ni baadhi ya changamoto zinazowakabili wanahabari sasa.
Amesema “endapo waandishi watatumia kalamu vizuri inaweza kuleta furaha na amani nchini lakini wakati huo huo inapotumika vibaya inaweza kuleta maafa. Ulimwengu umejaa hali ya kushindwa na kukosa, waandishi wanapaswa kuwa waadilifu kwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ili amani iendelee kuwepo” alisema Swai.
Pamoja na hayo amesea kwamba tasinia hiyo licha ya kuendelea kuboreshwa siku hadi siku wanahabari wanatakiwa kusahihisha semi zinazoendelea miongoni mwa watu ya kudhani kuwa habari ni habari mbaya tu na kuwataka waandishi kufanya kazi vizuri kwa kuweka dira nzuri kwa ajili ya baadaye.
Wakati huo huo muwasilisha mada katika mkutano huo mwandishi mkongwe na mahiri Fill Karashani ambaye aliwahi kupokea tunzo ya mwandishi bora aliwataka waandishi kuandika habari zenye tija kwa jamii ili kuisaidia serikali kufanya maamuzi sahihi na kuchukua hatua zinazofaa katika utendaji wake.
Alisema ugumu wa kuwapata wasemaji serikalini na kwenye taasisi binafsi, uelewa mdogo wa jamii juu ya waandishi, kukosekana kwa taasisi ya kutetea usalama wa waandishi ‘vibrant presure’ ni changamoto ambazo zimeendelea kuwepo ambazo pia waandishi wanapaswa kuzitafutia ufumbuzi.
Kwa upande wao waandishi wa habari wakichangia mada walitoa kero ambazo wamekuwa wakikutana nazo ambapo kwa upande wake Marietha Msembele alisema wamekuwa wakikutana na vitisho vya kurogwa na uadui kutoka kwa baadhi ya wadau wakati wanapotaka kupata ukweli wa mambo.
Mmoja wa wadau Francis Kalimba aliwataka waandishi kuacha kufanya kazi kama watumwa kwa kufuata kile wadau wanachotaka. Alisema waandishi wanapaswa kuandika ukweli wa mambo na kuepuka kuandika habari zenye ladha ya upendeleo.
Alisema “habari za michezo na zimejaribu kuipotezea heshima taaluma kutokana na kwamba wengi wanajaribu kuandika kwa kuegemea upendeleo wa, lakini pia waandishi wajitahidi kumiliki vitu vyao wenyewe yaani vitendea kazi. Pia waandike ukweli kuhusu mwelekeo wa taifa” alisema Kalimba.
No comments:
Post a Comment