Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, October 5, 2012

"KATIBU WA CCM ADONDOKA NA KUPOTEZA FAHAMU WAKATI WA KUHESABU KURA...!"

Katibu wa CCM Uchumi aliyemaliza muda wake wilayani Liwale mkoani Lindi, Said Lihomba amedondoka chini na kupoteza fahamu huku akitokwa na povu mdomoni, wakati akihesabu kura zake juzi katika uchaguzi wa ndani wa CCM.

Mpaka taarifa hizi tunazipata kutoka Lindi, zinasema Lihomba alikumbwa na masaibu hayo akiwa ndani ya chumba cha kuhesabia kura, baada ya kukataa kuchagua mwakilishi wa kumuhesabia kura na kuamua kwenda mwenyewe.

Awali kabla ya kutokewa na hali hiyo, Msimamizi wa Uchaguzi huo wilayani Liwale, Bi Farida Kikoleka aliwataka wagombea wa nafasi mbalimbali baada ya kupigwa kura, kutoa mwakilishi au kwenda wao wenyewe kuhakikisha kura zao katika chumba cha kuhesibia kura.

Kauli hiyo ya Bi Farida, ilisababisha wagombea wote wa nafasi hiyo, akiwemo Lihomba kwenda wenyewe kuhakikisha kura zao wakati zikihesabiwa.

Wagombea wengine walikuwa ni Mdai Mahela na Hamidu Likwa-watu.

Hata hivyo wakati wakihakiki kura zao, Lihomba aliyekuwa akipata kura chache huku Likwa-watu akiongoza kwa kura nyingi, alianguka ghafla chini. 

Kutokana na hali hiyo, wasimamizi wa uchaguzi huo, Bi Farida na Bwana Mathew waliamuru Lihomba atolewe katika chumba hicho na kumkimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Baada ya kumaliza kuhesabu kura, Bi Farida alimtangaza Likwa-watu kuwa mshindi wa nafasi hiyo baada ya kupata kura 58 na kufuatiwa na Mahela aliyepata kura 43 huku Lihomba aliyekuwa hospitalini akiambulia kura 10.

No comments:

Post a Comment