Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akifungua kikao cha Bodi ya
Barabara ya Mkoa wa Dar es salaam leo. Pamoja na mambo mengine amewataka
watendaji wa Halmashauri na Manispaa za jiji la Dar es salaam kusimamia
kikamilifu matumizi sahihi ya barabara ili kuondoa tatizo la msongamano wa
magari jijini Dar es salaam. Wengine wanaoonekana ni Mhe. Idd Azzan(Mb) Makamu
mwenyekiti wa Bodi ya Barabara mkoa wa Dar es salaam na Michael Mungaya kaimu
(kulia) Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam.
Washiriki
wa kikao cha Bodi ya Barabara ya mkoa wa Dar es salaam wakiwemo wakurugenzi wa
Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni wakifuatilia masuala mbalimbali
yaliyokuwa yakijadiliwa wakati wa kikao hicho leo jijini Dar es salaam.
Wajumbe
wa kikao hicho wakiwemo wakiwemo wabunge wa Dar es salaam Halima Mdee (CHADEMA)
jimbo la Kawe (wa kwanza kushoto nyuma) na Abbas Mtemvu Mbunge wa jimbo la
Temeke (CCM), wa pili kutoka kushoto mstari wa nyuma wakifuatilia taarifa
mbalimbali za utekelezaji wa miradi na maazimio ya vikao mbalimbali
vilivyofanyika.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa
kikao cha Bodi ya barabara kuhusu changamoto mbalimbali zinazoikabili manispaa
ya Kinondoni ikiwemo baadhi ya watu waliojenga maeneo yasiyoruhusiwa kutumia
vibaya uhuru wa mahakama kufungua kesi na kukwamisha uendelezaji wa baadhi ya
miradi ya barabara na ubomoaji wa baadhi ya nyumba zilizojengwa kinyumme cha
utaratibu jijini Dar es salaam.
Mbunge
wa jimbo la Kawe (CHADEMA) akichangia katika kikao cha Bodi ya Barabara ya mkoa
wa Dar es salaam leo jijini Dar es salaam na kutoa wito kwa watendaji wa
Halmashauri kusimamia ipasavyo makusanyo ya fedha ili kuziwezesha Halmashauri
kuboresha miundombinu jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya wilaya ya Temeke Bi. Magreth Nyalile akijibu baadhi ya
maswali yaliyoulizwa na washiriki wa kikao hicho wakiwemo wabunge kuhusu hatua
zinazochukuliwa na Halmashauri ya Temeke kujenga miundombinu na maegesho
yatakayotumiwa na malori yanayotoka bandarini na kupunguza kero kwa
watumiaji wengine wa barabara hizo kutokana na kushindwa kupitika kutokana na
msongamano wa malori hayo.
No comments:
Post a Comment