Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, October 20, 2012

MATAPELI WA MADINI WATIWA MBARONI BAADA YA KUMTAPELI MAMA MUUZA MBOGA...!


Matapeli wa madini wakiwa chini ya ulinzi wakipelekwa kituo cha polisi na askari ambaye jina lake halikuweza kupatikana kwa haraka.


Baadhi ya Matapeli wa madini waliosambaa sana mjini siku hizi wanaswa maeneo ya Kibo Commercial Complex Tegeta jijini Dar es saleem na askari polisi wakati wakiwa katika harakati za kumtapeli mama muuza mboga bila huruma. Matapeli hao wa madini walinaswa na camera ya mtandao huu katika eneo hilo la Tegeta, katika sakata hilo inasemekana kuwa kuna matapeli wengine walifanikiwa kukimbia kwa pikipiki, na kuwaacha wenzao waking'ang'aniwa na askari polisi waliokua wakifuatilia nyayo za matapeli hao tokea kitambo. Chanzo chetu cha uhakika kimebainisha kua matapeli hawa wakishatapeli wanabadilisha nguo na kuvaa nguo za kike ili wasitambulike na kuishia kutoka kuumiza muhanga wao wao, ila jana ndio ilikua 40 yao, baada ya juhudi za kumtapeli mama muuza mboga kugonga mwamba.

Chanzo: tina-sweethome1.blogspot.com

No comments:

Post a Comment