Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, October 25, 2012

MATENGENEZO YA RADA YAWA MAGUMU.!

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Fadhili Manongi

Kifaa kimojawapo cha rada inayotumika kuongozea ndege katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) iliyokuwa katika matengenezo baada ya kuharibika, kimepelekwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matengenezo zaidi baada ya kushindikana kutengenezeka hapa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Fadhili Manongi, alisema jana kuwa mtaalamu kutoka Afrika Kusini aliyekuwa anaifanyia uchunguzi rada hiyo ameondoka na kifaa kilichopata hitilafu kiitwacho 'Sensor' kwenda nchini humo kwa matengenezo.

Alisema endapo kifaa hicho kitashindika kutengenezeka kitanunuliwa kingine na kupachikwa katika rada hiyo.

“Tatizo ni dogo, ni kifaa kimeshindikanika kutengenezeka, mtaalamu ameondoka nacho leo asubuhi kwenda Afrika Kusini kwa matengenezo, ikishindikana tutanunua kingine, ndani ya siku mbili tutakuwa tumekamilisha tatizo hilo,” alisema Manongi.

Manongi alisema tatizo kubwa linalosababisha rada hiyo kupata hitilafu ya mara kwa mara ni umeme unaokuja kwa kasi na kusababisha baadhi ya vifaa vyake kuungua.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, rada hiyo kwa sasa imeshakufa na haifai kutengenezeka na hata ikitengenezeka itakuwa inaharibika kila wakati.

Mwanzoni mwa mwiki hii,Manongi aliliambia NIPASHE kuwa rada hiyo ilikuwa katika matengenezo ya mwisho na ilitarajiwa kuwashwa majira ya jioni kufuatia mtaalamu kutoka Afrika Kusini kuifanyia ukaguzi wa mwisho.

Matengenezo ya rada hiyo yalianza Oktoba 12, yakifanywa na mtaalamu kutoka nchini Kenya akisaidiana na mtaalamu huyo kutoka Afrika Kusini, yalitarajiwa kumalizika Oktoba 21, mwaka huu, lakini imeshindikana.

Rada hiyo iliharibika kufuatia kifaa kinachotumika kusambazia umeme kiitwacho UPS au “Uninterrupted Power Suply” kuungua zaidi ya wiki mbili iliyopita.

Aidha, tatizo ndani ya rada hiyo lilianza kuonekana tangu siku walipoifanyia ukarabati Agosti 18, mwaka huu, kwa kuanza kuonyesha taa nyekundu ikiashiria kuna hitilafu ndani ya chombo hicho.

Hii ni mara ya pili kwa rada hiyo kuharibika. Mara ya kwanza Agosti 3, iliharibika na kuthibitishwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Agosti 23 mwaka huu, ambaye aliutangazia umma kupitia mkutano aliouitisha na vyombo vya habari na kusema kuwa rada imeharibika.

Baada ya matengenezo hayo, Oktoba 12, mwaka huu rada hiyo iliharibika tena.

No comments:

Post a Comment