MAMLAKA ya Majisafi na taka Manispaa
ya Musoma mkoani wa Mara (MUWASA) imewashusha waandishI wa habari njiani
waliokuwa katika ziara ya Naibu waziri wa maji na umwagiliaji Dk.Eng.Binilith
Mahenge kwa madai ya kisingizio cha ufinyo wa
bajeti.
Baadhi ya Waandishi wa habari wa
magezeti ya mbalimbali mkoani hapa wameshushwa katika eneo la ofisi ya Mkuu wa
wilaya ya Manispaa ya Musoma na Afisa Mahusiano wa
Mamlaka hiyo Emmanuel Ruyobya hali ambayo ni
imeonekana kuwa ni udhalilishaji.
“Kiukweli huu ni udhalilishaji
kwani sisi tuna vyombo vyetu ambavyo tunavifanyia kazi na si lazima tulipwe
posho sasa huyu yeye anasema bajeti finyu wakati sisi hatujaomba posho” alisema
mmoja wa waandishi wa
habari walioshushwa katika gari hiyo.
Akisoma taarifa ya
Maendeleo na Changamoto zake katika ofisi ya mkuu wa mkoa kwa Naibu,Katibu
Tawala wa mkoa hupo Climent Lujaji alimuagiza mkurugenzi wa MUWASA Genes Kaduri
kuwaweza waandishi hao katika suala la usafiri ili waweze kushiriki katika ziara
hiyo ambapo mkurugenzi huyo alimkubalia .
Aidha Baada ya kuondoka katika eneo
la ofisi wa mkoa waandishi wa habari hao walishishwa katika gari hiyo kwa madai
hayo na kwamba wameishaalika waandishi wao .
“Kama
Katibu Tawala wa mkoa ndiye kawaambia muje
nendeni awalipe na kuwatafutia usafiri.,alisema Afisa
mahusiano Ruyobya kwa jaziba kubwa.
Tabia ya kuwashusha waandishi wa
habari si la mara ya kwanza katika ziara mbalimbali zinazofanywa
na viongozi kama hao mkoani hapa hususani katika vyombo habari vya
magazeti kubaguliwa na hata hivi karibuni 5 Oktoba mwaka
huu imefanyika ziara ya Naibu waziri wa Nishati na Madini Stephen
Masele ambapo pia vyombo vingine vimebaguliwa.
Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Binilith Mahenge
ameaza ziara yake ya kujua maendeleo na changamoto zake
mkoa wa Mara ambapo imeanzia katika halmashauri ya wilaya
ya Manispaa ya Musoma,Butiama kukagua chanzo cha maji cha Mugango
–Kiabakari, Rorya,Serengeti na kumalizia wilaya ya Bunda.
No comments:
Post a Comment