Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, October 11, 2012

MGOMBEA WA UDIWANI KWA TIKETI YA CHAMA CHA CHADEMA ATAKA KUJIENGUA KWENYE KINYANG'ANYIRO HICHO...!

Mgombea wa chama cha Chadema katika uchaguzi wa nafasi ya udiwani kata`ya Luwumbu wilayani Makete amekanusha kujitoa katika kinyanyang'anyiro hicho, nakuseme hizo ni propaganda za chama cha mapinduzi CCM.

Mwenyekiti wa Chadema Wilayani Makete Bw Shabani Mkakanze alisema CCM walimfuata mgombea wao na kumwahidi pesa na ajira ili ajitoe kugombea nafasi hiyo kwa kuwa wanajua chama chao kina nguvu.

Alisema hizo ni propaganda kutokana na CCM kumsimamisha mgombea ambaye anatuhumiwa kwa ufisadi katika kanisa la KKKT Dayosisi ya kusini kati  na wanauhakika wa kushida kwa kishindo katika uchaguzi huo.

Mkakanze alisema kwa sasa chama chake kimenza kampeni na wanategemea kupata nguvu kutoka kwa viongozi wa taifa wa chama chao.

Kwa upande wao CCM Makete kupitia katibu wake Bw Miraji Mtaturu alisema kuhusu kujitoa kwa mgombea wa Chadema ametumia busara kwa kutambua kuwa chama chake hakiungwi mkono na wananchi na kusema chama cha CCM hakihusiki na kumrubuni mgombea wa chadema.

"Sisi tunajiamini na wao wametugwaya kwa kuwa hawakubaliki na wanautambua moto wa CCM, ya nini tumrubuni, hawana sera hawa CHADEMA, tena hawana jipya ndugu mwandishi" alisema Mtaturu

Kuhusu mgombea wake kutuhumiwa kwa ufisadi alisema ;Chadema wanatapa tapa kwakuwa wanajua Luwumbu ni ngome yao kubwa na katika uchaguzi mkuu uliopita CCM ilipita bila kupingwa kwa hiyo kma wana uhakika kuwa mgombea wao alikuwa fisadi ndani ya kanisa kwa nini hakushatakiwa?Naye msimamizi  wa uchaguzi huo mdogo Bw Jeremia Chalamila alisema mgombea wa Chadema Raphael Kyando hajajitoa kugombea kiti cha udiwani na amesha kanusha uvumi huo kwa kuindikia Tume barua.

Chalamila alisema kwa sasa majina mawili ya wagombea wameshayapeleka kwenye tume ya uchaguzi na suala la kujitoa kwa mgombea wa Chadema ni uvumi kutoka chama kingine(hakukitaja) kwa kuwa mgombea wa chadema amekanusha uvumi huo kwa maandishi.

Aidha Chalamila alisema kuhusu pingamizi lililowekwa na CCM kuhusu mgombea wa Chadema kuwa hakutimiza masharti ya kudhaminiwa kwa kudhaminiwa na watu ambao sio wakazi wa eneo hilo limetupiliwa mbali na tayari CCM wameshajulishwa.

Uchaguzi mdogo katika kata ya Luwumbu unatarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu kufutia kifo cha aliyekuwa Diwani wa kata hiyo Bw Dominiki Tweve (CCM) na CCM imemsimamisha Mch. Enocki Ngajilo na kwa upande wa Chadema imemsimamisha Bw Raphael Kyando.

No comments:

Post a Comment