*DR. SLAA AMECHANGANYIKIWA: Nape
*Adai amekubuhu kwa utapeli wa kisiasa
*Amtuhumu kuiua Chadema
*Asema si M4C tena bali ni M4D
Tarehe
28/10/2012 kumefanyika uchaguzi mdogo katika kata 29 kwenye mikoa
mbalimbali nchini. Kata hizi zilikuwa wazi kwa sababu mbalimbali, hivyo
kwa mujibu wa sheria ililazimika kufanya uchaguzi mdogo kujaza nafasi
wazi.
Ukiacha
matukio kadhaa ya vurugu, maeneo mengi uchaguzi umeenda kwa utulivu.
Chama Cha Mapinduzi kinawapongeza wote waliofanya uchaguzi kwa amani na
utulivu, huo ndio utamaduni wa watanzania, kushindana bila kupigana.
Muhutasari
wa matokeo ya jumla unaonyesha kuwa TLP wameshinda kata moja(1), CUF
wameshinda kata moja(1), CHADEMA wameshinda kata 5 na CCM imeshinda kata
ishirini na mbili(22).
Kwa
matokeo haya ambayo kwakweli yanatafisiri pana sana hasa ikizingatiwa
kuwa mgawanyo wa kata ulikuwa nchi nzima basi matokeo haya yanatoa
ujumbe wa jinsi CCM inavyokubalika nchini kwasasa.
Na
pia ni uthibitisho wa kile kilichoitwa M4C(movement for change) kwa
Chadema kuwa ni kiini macho kisichokuwa na matunda chanya bali ni M4D (
movement for dealth). Na hii inatokana na aina ya siasa za hovyo
zinazoambatana na operesheni hii. Bila shaka sauti ya Watanzania kwa
aina hii ya siasa imesikika bila kumumunya maneno.
Aidha
kwa upande mwingine siasa za uongo,uzushi na ulaghai zilizotumiwa na
vyama vya upinzani hasa Dr. Slaa kwenye kampeni hizo imekidhalilisha
chama hicho na kudhalilisha utu uzima wa Katibu Mkuu huyo wa Chadema.
Mfano
mzuri ni pale ambapo Dr. Slaa bila ya soni alipoamua kumzushia Rais na
Mwenyekiti wa CCM kuwa kasafiri mpaka China eti kwenda kumuokoa mwanae
ambaye kwa madai ya Dk. Slaa alikamatwa na madawa ya kulevya nchini
humo.
Bila
aibu Dr. Slaa alizusha uongo huo Tabora kwa wapiga kura huku akijua
kuwa ni uongo, lakini hata hivyo uongo huo hauna sehemu kwenye kampeni
hizo za udiwani. Wananchi walitegemea kusikia namna ya kutatua kero zao
badala yake wakashuhudia mtu mzima akizusha ujinga wa ajabu.
Uongo
huu na mwingine mwingi unathibitisha kuwa Dr. Slaa anazeeka vibaya
kwani kila anavyoongeza siku hamu na tamaa yake ya kusema uongo ili
kujiongezea umaarufu na kujenga chuki kati ya watanzania inaongezeka
sana. Hakika TAPELI HUYU WA KISIASA, LICHA YA KUZEEKA VIBAYA SASA
ANACHANGANYIKIWA.
Naamini
mzigo aliotwishwa na wenzake unamlemea sana, hivyo namshauri awaachie
vijana wajaribu kukiokoa chama hicho kinachoporomoka kwa kasi,
vinginevyo wana Chadema waanze kuandaa matanga kwa chama chao.
Ukitazama
mgawanyo wa ushindi huu utagundua kuwa, pamoja na Katibu Mkuu wa
Chadema Dr. Slaa kwenda na kupiga kambi kanda ya ziwa ameambulia kata
sifuri(0). Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa kutumia gari ya
serikali alijikita kusini nako katoka kapa.
Nguvu
iliyotumika kutoka kwa vyama vya upinzani hasa Chadema hailingani na
ushindi walioupata. Wakati CCM ikiwa busy na chaguzi za ndani ya Chama
wao wamezungusha viongozi wa kitaifa nchi nzima na matokeo ndio hayo.
Tunawashukuru
sana Watanzania kokote nchini walioendelea kutuamini na kutupa dhamana
ya kuendelea kuwaongoza na kutekeleza ilani yetu. Tunawaahidi utumishi
uliotukuka.
Chanzo ::http://daresalaam-yetu.blogspot.com
No comments:
Post a Comment