Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, October 5, 2012

NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI ZASHAURIWA KUTODHARAU LUGHA YA KISWAHILI

Nchi za Afrika Mashariki zimeshauriwa kuondoa kasumba iliyopo hivi sasa ya kuidharau lugha ya Kiswahili na badala yake ziitumie lugha hiyo kama mkombozi katika kuziunganisha nchi hizo.

Ushauri huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Aldin Mutembei, katika Mkutano wa Kimataifa wa miaka 50 ya Kiswahili unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema lugha ya Kiswahili imeshuka kutokana na watu wengi kutokuwa na ujasiri wa kuizungumza tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

“Ujasiri wa kuzungumza Kiswahili uliokuwapo zamani enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hivi sasa haupo, na hii ni kutokana na kasumba na mwingiliano wa lugha za kigeni. Tunahitaji kubadilika na kuifanya lugha hiyo iwe ya umoja katika afrika,” alisema.

Alisema wana mpango wa kuendesha semina kwa walimu kuhusu umuhimu wa Kiswahili, kwa lengo la kuongeza hamasa ya kutumia lugha hiyo shuleni.
 
Aliishauri serikali kuanzisha mfumo mpya wa kutumia lugha ya Kiswahili kuanzia ngazi ya elimu ya awali mpaka vyuo vikuu.

“Hatupingi kwamba, lugha nyingine zisitumike, lakini tunataka Kiswahili kiwe na hadhi ya Kimataifa,” alisem
a.

No comments:

Post a Comment