Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, October 28, 2012

POLISI WAKAMATA UJUMBE MFUPI WA SIMU KWA AJILI YA KUTEKELEAZA MAUAJI YA KAMANDA BARLOW...!

Siku moja baada ya Jeshi la Polisi kutoa taarifa ya awali ya uchunguzi wa mauaji ya kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, ujumbe mfupi wa simu ya mkononi kwa ajili ya kutekeleza mauaji hayo imenaswa.

Kamanda Barlow aliuawa usiku wa manane alipokuwa akitoka kwenye kikao cha harusi ya ndugu yake. Alifikwa na mauti hayo baada ya kupigwa risasi akimsindikiza Mwalimu Doroth Moses.


Habari zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya makachero jijini Mwanza zinaeleza kuwa, ukweli wa mauaji hayo umebainika na kwamba watuhumiwa waliokamatwa wanahusika moja kwa moja na mpango kamili wa mauaji hayo.


Kwa mujibu wa taarifa hizo, inadaiwa kuwa Kamanda aliuawa baada ya mmoja wa wahalifu aliyekuwa akikabiliwa na kesi nzito (jina tunalihifadhi) kutoa kiasi cha fedha kupitia kwa mtu wake wa karibu ili kutekeleza mpango wa mauaji ya kulipiza kisasi.


Kupatikana kwa wauaji hao, kumetokana na simu ya Mwalimu Dorothy Moses kupitia ujumbe wa simu aliokuwa akiwasiliana na wahusika.

Hata hivyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Lilian Matola alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alisema taarifa siyo za kweli na kusisitiza kwamba taarifa aliyoitoa DCI Robert Manumba ndiyo sahihi.


"Haya mambo yanatoka wapi, kwanza siyo kweli hata kidogo, hawa ni watu walikuwa kwenye safari zao za uhalifu ndipo wakakutana na Kamanda Barlow," alisema.


Habari hizo zinaeleza kuwa, kubainika kwa mpango huo ni baada ya kunasa ujumbe mfupi wa maandishi uliokuwa ukionyesha matukio yote tangu walipokuwa hotelini na kwamba wakati wote wauaji walikuwa wakipewa taarifa za kila nyendo za Kamanda Barlow.


Ujumbe mmojawapo ulionaswa katika moja ya simu unasema, “Nipo kijiweni kwangu…. nitawajulisha zaidi”.


Alisema kutokana na kubainika kwa ujumbe huo wa maandishi wa simu, jeshi hilo limelazimika kufuatilia matukio kadhaa yaliyomo katika historia ya mtuhumiwa.


Kuhusu kauli ya Manumba alisema kuwa, kama DCI Manumba alitoa taarifa yake kwa lengo la kiintelejensia kwa ajili ya kusaidia upelelezi anakubaliana na hilo.”


“Unajua kuna mbinu nyingi za upelelezi, inawezekana wameeleza hayo ili kuwazubaisha watuhumiwa kisha uchunguzi wa kina ukaendelea, hapo ni sawa, lakini kama ndiyo mwelekeo wa uchunguzi wao, basi wanapaswa kujua kuwa wameacha vitu vingi sana vya msingi,” alieleza askari mwingine.

DCI Manumba katika taarifa yake, alisema kwamba Jeshi la Polisi limewatia mbaroni watu watano jijini Dar es Salaam wakiwa na bunduki aina ya shortgun inayodaiwa kutumika katika mauaji hayo. Hata hivyo walishindwa kubainisha sababu za mauaji hayo licha ya kueleza kuwa watuhumiwa waliokamatwa walikiri kuhusika.


Akielezea chanzo cha mauaji hayo kutobainika, Inspekta Generali wa Polisi, IGP, Said Mwema alisema jeshi lake pamoja na kuwakamata watu watano jijini Dar es Salaam wanaosadikiwa kuwa majambazi, bado wanafanya uchuguzi wa chanzo cha mauaji hayo ili kujua kama majambazi hao walikutana na kamanda kwa bahati mbaya katika kazi zao au la.

Alisema, mbali na kuwakamata watuhumiwa hao watano na kukiri pamoja na kuonyesha bunduki aina ya shortgun waliyotumia kwa mauaji, watuhumiwa wengine wawili bado wanasakwa pamoja na redio ya mawimbi ya kamanda huyo ambayo iliibiwa eneo la tukio yalikotokea mauaji. 


Chanzo : Mwananachi

No comments:

Post a Comment