Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, October 2, 2012

RUFAA YA ALIYEKUWA MBUNGE WA JIMBO LA ARUSHA MJINI LEMA YASHINDWA KUSIKILIZWA BAADA YA KUIBUKA HOJA ZAIDI YA N...!ANE

 Aliyekuwa  mbunge wajimbo la Arusha Mjini Godbless Lema akiwasalimu wanachama mara baada ya kutoka mahakamani
 
 Wananchi waliomsindikiza lema  mahakamani.
 
Lema akiwajuu ya gari anawapungia wananchi wakati akitokea mahakamani

Lema akiwa anatoka mahakamani leo 
 
RUFAA  ya  aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema imeshindwa kusikilizwa  baada ya  kuibuka kwa hoja zaidi ya nne ambazo zimewasilishwa na upande wa mawakili wa CCM  na kusababisha kesi hiyo kuahirishwa hadi tarehe itakayopangwa  tena na mahakama ya Rufaa.

Hoja hizo ziliibuliwa na  wakili wa ccm ,Alute Mughwai akisaidiwa na wakili wa serikali Modest Akida wanaowawakilisha  wajibu rufani ambao ni Agness Mollel, Happy Kivuyo na Musa Mkanga .

Hoja hizo zilianza kutolewa na  wakili wa wajibu rufani ,Mughwai kudai kuwa rufaa iliyokatwa na Lema kupitia kwa mawakili wake, Method Kimomogoro pamoja na Tundu Lissu imekosewa kwa kukiuka kanuni za mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu pia katika rufaa hiyo hakuna mhuri wa mahakama wala tarehe .

Alihoji ni kwanini Lema akimbilie kukata rufaa ndani ya siku 29 badala ya siku 60 kwani hajapitia nakala ya hukumu ya awali hivyo endapo angepitia hukumu hiyo pamoja na mawakili wake angeweza kujua kunamatatizo gani na ayarekebishe badala yake wamekata rufaa bila
kuangalia kasoro zilizojitokeza.

Alisema ni lazima muhuri wa mahakama uwe pamoja na tarehe na kutokana na umuhumi wa mhuri ndio maana hata mtu wa kijijini anaposhtakiwa au kuhitaji msaada sehemu muhimu inabidi aende kwa mtendaji wa kijiji kupata barua yenye mhuri na kuhoji ni kwanini Lema amekimbilia kukata rufaa bila kuangalia kasoro zilizopo na kutoa rai kwa jopo la majaji
hao kutupilia mbali rufani hiyo ya Lema kwasababu haikakidhi matakwa ya kisheria.

‘’Kwanini mmekimbili kukata rufaa bila kukagua kama kunakasoro katika rufaa hii hivyo naomba jopo hili la majaji litupilie mbali rufaa hii na Lema alipe fidia ya kesi hii,kwani kabla ya kukimbilia mahakamani ni vema angehakiki nakala ya hukumu ndipo aje kufungua kesi na
kwatatizo hili naomba mahakama hii kutupilia mbali rufaa hii na Lema ajipange upya’’.

Nao  Wakili wa Lema ,Kimomogolo alisema makosa yaliyotokea ni ya kibinadamu na yamefanywa na mahakama na si Lema wala mawakili wao hivyo aliwasihi majaji hao kutotupilia mbali rufani yao kwani katika kesi kama hiyo ni lazima makosa madogo madogo yatokee na kusisitiza mahakama kutenda haki kwa Lema.

Kimomogoro aliendelea kusema kuwa ikiwa wakili Mughwai alipewa ushindi na mahakama kuu Kanda ya arusha hakupewa nakala ya hukumu iliyosahihi je yeye aliyeshindwa angweza kuipata vipi nakala hiyo na kugundua kasoro zilizopo na kuongeza kuwa mara baada ya hukumu jalada la kesi hiyo lilipelekwa kwa Msajili wa  Mahakama ya Rufaa na pia walikuwa
wakipata taarifa nusunusu kutokana na kutokuwa na jadala hilo karibu hivyo walishindwa kufuatilia .

Naye Wakili wa Serikali Timon Vitalis alisema anaounga mkoni hoja za Kimomogoro za kutaka rufaa hiyo isikilizwe kwani tatizo lililojitokeza kwenye hoja za wakili Mughwai si la Lema wala mawakili wake bali tatizo ni la kimahakama hivyo mkata rufaa asiadhibiwe kwa kosa ambalo
si lao.

Alisema mahakama ndio inayopaswa kulalamikiwa katika kasoro zilizojitokeza na si mkata rufaa na kuhusu hoja iliyotolewa na Mughwai kuwa Lema achapwe fimbo kutokana na kasoro hizo aliongeza si sahihi kwani mahakama si  sungusungu bali inasimamia na kutoa haki hivyo
aliwasihi majaji hao kuzipuuza pingamizi za kinaMughwai.

Naye Majaji ,salum Massati,Natalia Kimario  wakiongozwa na Jaji  Mkuu, Mohammed Chande Othman  waliahirisha kesi hiyo hadi tarehe itakayopangwa .

Baada ya kuahirisha kesi hiyo ,JAJI Mohammed Chande Othman alishukuru wananchi  waliojitokeza kusikiliza kesi mbalimbali katika mahakama ya Rufaa na kuongeza kuwa mahakama hiyo ilianza usikilizwaji wa rufaa mbalimbali Septemba 3 hadi Oktoba 2 mwaka huu.

Alisema katika kikao hiki wamesikiliza mashauri 36  na  katika vikao vitatu vya mahakama ya rufaa wamesikiliza jumla ya mashauri 112 na Arusha bado inamashauri mengi yakusikilizwa hivyo alidai kuwa watajitahidi kupanga tarehe za mapema ili waweze kusikiliza mashauri
hayo na kuwashukuru polisi,magereza ,mawakili pamoja na wale wote walioshiriki kufanikisha vikao hivyo.

Nje ya Mahakama ,umati wa watu uliokusanyika mahakamani hapo, waliokuwa wameshika matawi ya miti walitawanyika kwa maandamano huku wakipaza sauti ya People’s Power na kutaka uchaguzi urudiwe ili waweze kupata mbunge katika Jimbo hilo.

No comments:

Post a Comment