Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, October 2, 2012

MWENYEKITI MOSHI AKERWA NA WAKUU WA IDARA...!

MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro Moris
Makoi, amewaonya wakuu wa idara kuacha tabia ya kuhodhi mafuta na
kutumia magari ya halmashauri hiyo kutokana na mali hizo kupatikana
kwa fedha za walipa kodi.

Amesema kuwa wakuu wa idara wamekuwa wakijichukulia madaraka ya
ukurugenzi na kujisainishia vibali vya kujaza mafuta kwenye magari
hayo na kuyatumia katika shughuli zao binafsi.

Ameyatanabaisha hayo hivi karibuni katika kikao cha baraza la madiwani
wa halmashauri hiyo wakati akihitimisha kikao hicho na kufafanua
kuwa,hiyo ni kero kubwa iliyopo katika halmashauri hiyo na ndiyo
inayochangia kuwapo kwa uzembe kazini kutokana na kutumia mali hizo
pasipo kibali maalumu.

Ameongeza kuwa kufuatia tabia hiyo kumekuwa na malalamiko kutoka kwa
wanannchi kuwa wakuu hao wa idara wanavuja mali za umma jambo ambalo
limekuwa ni kero kubwa kwao

Aidha  amesisitiza Umuhimu wa kutunza rasilimali na  mali ya umma
kutokana na mali hizo kupatikana kutokana na nguvu kazi za wananchi
ambazo ni kulipa kodi kwa serikali na halmashauri kwa ujumla


Katika hatua nyingine,madiwani wa halmashauri hiyo wameunga mkono onyo
hilo la Mwenyekiti na kusema kuwa mbali na aina mpya ya ubadhirifu,pia
ni utovu na wizi wa nguvu za wananchi.

No comments:

Post a Comment