Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, October 21, 2012

SOPHIA SIMBA ACHAGULIWA TENA KUWA MWENYEKITI WA UWT...!

Sophia Simba, amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), amekuwa akisemwa wakati mwingine kwa mafumbo kuhusu masuala ya mahusiano ya kimapenzi aliyopata kuwa nayo. Katika mahojiano na RAIA MWEMA, mama huyo, miongoni mwa mambo mengine, aliamua kuwa muwazi juu ya mahusiano hayo na pia masuala kadhaa yanayohusu UWT. 

Raia Mwema: Wasomaji wetu wangependa kukufahamu kwa sababu mengi yamekuwa yakisemwa na yakinong’onwa hususan kuhusu elimu yako; labda kwa vile hawaifahamu vizuri. Unaweza kutupa CV yako kwa kifupi?

 Mama Sophia Simba: Asante kwa kunipa nafasi hii adimu. Nimefurahi kwamba umeweza kufika ofisini kwangu na kuweza kuongea na mimi. Nashukuru kwamba umeona upo umuhimu wa watu kunijua mimi Sophia ni nani hasa. 

Ni kweli maneno mengi yamekuwa yakisemwa ambayo hayapendezi, lakini nitafanyaje? Kwa hiyo, kwa kifupi sana ningependa nikufahamishe labda pengine kwa kupitia wewe watu watanifahamu. 

Mimi naitwa Sophia Simba. Ni Sophia Mathew Simba. Nyambi ni jina langu la nyumbani. Wazaramo wana majina yao ya ukoo, kwa hiyo mimi ni Nyambi na mdogo wangu alipewa jina lingine. Nilipokuwa mdogo baba yangu akasema .... Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com

No comments:

Post a Comment