Taarifa hiyo imetolewa na kaimu meneja mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano (TCRA) Semu Mwakyanjala ambaye amesema mamlaka hiyo itaanza kwa kutoa elimu kwa umma kuhusiana na umuhimu wa kununua simu original.
Akiongea na chanzo cha mtandao huu alisema kuwa hatua hiyo itachukuliwa na nchi zote wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki zikiwemo Rwanda, Uganda na Burundi.
Kuna taarifa kuwa makampuni mengi ya simu nchini Tanzania yameupokea mpango huo kwa shingo upande kwa hofu kuwa yatapoteza wateja wengi.
Kwa upande wa tume ya mawasiliano ya Uganda (UCC) hatua hiyo ya kuzima simu bandia itafanyika mwishoni mwa mwezi November.
No comments:
Post a Comment