Baada ya vifo vyao ukweli ndio
umejulikana kwamba wanachuo hao hawakuwa wezi bali walisingiziwa,
kutokana na hilo wanachuo wenzao wenye hasira waliingia mtaani kwenye
kijiji cha Aluu ili kulipa kisasi.
Wamechoma moto nyumba kadhaa,
wamechukua mali za watu wakiwemo wafanyabiashara pamoja na pesa zao na
kufanya uharibifu mwingine na fujo juu ikiwa ni kulipa kisasi kwa
wananchi wa kijiji hicho ambacho hivi karibuni kimekua kikikumbwa na
matukio ya uhalifu ndio maana ilikua rahisi kuamini pia vijana hao wanne
walikua wezi ambapo wakazi wa kijiji cha Aluu walihama makazi yao kwa
kukimbia baada ya kusikia kundi la wanachuo hao likija kwa nguvu.
No comments:
Post a Comment