Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, October 15, 2012

TCRA YATWAA TUZO YA UBINGWA SEKTA ZA FEDHA NCHINI...!

Mstahiki Meya wa Ilala, Mhe. Jerry Slaa, akimkabidhi cheti cha Ushindi wa Jumla, Kaimu Meneja Mawasiliano wa TCRA, Semu Mwakyanjala
*******
Na  Pascal Mayalla.
Mamlaka ya Mawasiliano Nchini, TCRA,  imeshinda Tuzo ya Tasisi Bora ya Mawasiliano ya Kifedha  nchini, baada ya kuibuka na ushindi wa jumla kwenye maonyesho ya Seta ya Fedha nchini, yaliyomalika jana, kwenye viwanja vya  Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.

Ushindi huo wa TCRA, umepatikana kufuatia  makampuni , Asasi na  Tasisi za kifedha nchini, zilizoshiriki katika maonysho hayo, kupimwa jinsi huduma zake zinavyosaidia ukuaji wa sekta ya fedha nchini, ambapo TCRA  imeibuka na ushindi  huo  kufuatia kutoa vibali na number maalum kwa makampuni ya simu na taasisi za kifedha nchini kutumia number number hizo kwa huduma za kifedha,  ziitwazo SIM Banking, kulikopekea Watanzania wengi zaidi kufikiwa na huduma za kifedha kwa njia ya rahisi zaidi .

Ushindi wa pili umetwaliwa na kampuni ya simu za mkoni ya Vodacom kupitia huduma yake ya M-Pesa ikielezewa hii ndio huduma ya pesa iliyosambaa nchini kote na kutumiwa na mamilioni ya Watanzania kama mkombozi wao katika huduma za kifedha.

Kwa upande wa mabenki, Benki ya CRDB ndio imeshinda kama benki kiongozi katika maonyesho hayo kwa kuwa ndio benki pekee hapa nchini, iliyoshiriki maonyesho hayo kwa kishindo kikubwa kwa kuwakilishwa na benki yenyewe ya CRDB PLC  na kampuni yake tanzu ya CRDB Microfinance LTD iliyoelezwa  kuwa ndio benki pekee iliuyowafikia wajasiliamali wadodo wadogo wa vijini kuliko benki nyingine yoyote.

Akielezea,  ushindi huo una maan a gani kwa TCRA, Mkuu wa Huduma za Elimu kwa Umma wa CRDB,  Issack Mruma, amesema ushindi huo  ni motisha kwa TCRA kuzidi kutoa huduma bora zaidi za mawasiliano nchini na kueleza umekuja wakati muafaka na sambamba na Tanzania kuchaguliwa kuingia kwenye Bodi ya Shirika la Posta Ulimwenguni UPU katika mkutano unaendeleo huko Doha, Falme za Kiarabu.

Akipokea Tuzo hiyo,  Kaimu Meneja Mawasiliano wa TCRA,  Semu Mwakiyanjala, amesema ushindi huo, unawapa faraja angalau kwa TCRA kutambulika nyumbani kuwa ni mabingwa wa maendeleo ya sekta ya mawasiliano sio nchini tuu bali barani Afrika.

“Unajua Nabii huwa hathaminiwi nyumbani, sisi TCRA tunaongoza sana katika huduma bora za mawasiliano  barani Afrika na duniani kwa ujumla, nchi nyingi zinakuja kujifunza kwetu,  hati kazi ya upangaji wa maswafa dunuani, TCRA inategemewa sana kuwapangia masafa nchi nyingine kule kwenye  ITU” alisema Mwakiyanjala.

Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa TCRA na Mstahiki Meya wa Ilala, Mhe. Jerry Slaa, aliyekuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha maadhimisho hayo baada ya maonyesho ya siku nne ya taasisi za fedha nchini yaliyoandaliwa na kampuni ya Neubrand.

No comments:

Post a Comment