Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, October 4, 2012

VIFO VYA ONGEZEKA KWENYE AJALI ILIYOTOKEA MBEYA...!

Mbunge wa Viti Maalum, Dk Mary Mwanjelwa akiagwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro jana kabla ya kusafirishwa kwa ndege hadi jijini Dar es Salaam. Dk. Mwanjelwa alihamishiwa Hospitali ya

Idadiya watu waliokufa katika ajali ya lori la mafuta  lililogonga magari  manne  na kuteketea kwa moto mkoani Mbeya imeongezeka na kufikia 11 baada ya majeruhi mmoja  aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kufariki dunia.

Aidha, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa, amehamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi kutoka Hospitali Teule ya Ifisi alikokuwa amelazwa.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, alisema mbunge huyo alisafirishwa pamoja na dereva wake, Rajabu Majuto, kwenda Muhimbili jana  alasiri kwa ndege ya kukodi aina  ya 5-H-AAA, Auric Air mali ya kampuni ya Coastal Air.

Mkurugenzi wa Mipango katika Ofisi za Bunge, Siegfried Kuwite, alisema Dk. Mwanjelwa baada ya kupokelewa angeanza kupatiwa matibabu.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, alisema idadi ya waliokufa imeongezeka na kufikia 11 ambapo baadhi wametambuliwa na wengine bado.

Alisema majeruhi aliyekufa aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya  ametambuliwa kwa jina la Njole Sande.

Maiti wengine waliotambuliwa ni  Justin Kabasa (22) mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofili Kisanji (TEKU) na askari wa kituo kidogo cha polisi Mbalizi PC Samson Masunga.

Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Thomas Isidory, alisema maiti tisa wa ajali hiyo  zimetambuliwa, lakini hazijachukuliwa na  ndugu.

Isidory alitaja maiti zilizotambuliwa na kuchukuliwa ni pamoja na aliyekuwa katibu wa Mbunge Dk. Mwanjelwa, Amina Mwampashi, mkazi wa wilaya ya Ileje mkoani Mbeya.

Wengine ni Limston  Mwanyama aliyetambuliwa miguu, kidevu na kipande cha shati ni mkazi wa uyole, Asnati Wega, Anjela Mashauri, Marlon Mwakabungu, Patrick Mbilinyi, pamoja na miguu miwili isiyokuwa na kiwiliwili ambayo haijafahamika ni ya nani.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali Teule ya Ifisi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeyta Vijijini, Dk. Msafiri Kimario, alisema majeruhi nane waliokuwa wamelazwa katika hospitali hiyo  watano wameruhusiwa na kubakia watatu ambao wanaendelea na matibabu.

Wakati huo huo  Rais Jakaya  Kikwete amewatuma salamu za rambirambi kwa Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Shinyanga kufuatia ajali zilizotokea juzi mikoani humo kwa nyakati tofauti.

“Nimepokea kwa mshtuko mkubwa, habari za ajali za kusikitisha za ajali mbaya mkoani mwako. Nakupa pole kwa ajali hiyo ambayo imesababisha msiba mkubwa mkoani mwako na kuleta simanzi na huzuni kubwa, sisi sote tumehuzunishwa na kushtushwa” amesema katika salama alizomtumia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ali Rufunga.

Rais pia amewataka viongozi wote  kutochoka kuwakumbusha raia, wamiliki wa vyombo vya usafiri  na madereva kuwa waangalifu na makini wakati wanapokuwa safarini  kwani  usalama barabarani  ni jambo  muhimu sana wakati wanapokuwa  barabarani.

Juzi lori la mafuta lenye namba T 911 BUV na tela lake T  841  BTC  lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) lilifeli breki na kuyagonga magari manne ikiwemo basi dogo la abiria Toyota Hiace lenye namba  T 887 AHT na kusababisha vifo vya watu 11.

No comments:

Post a Comment