Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, October 12, 2012

VURUGU ZATOKEA MBAGALA KIZUIANI BAADA YA KIJANA KUDAIWA KUKOJOLEA QURAN


Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba kuna vurugu zinaendelea eneo la Mbagala Kizuiani ambapo baadhi ya Waislamu wameandamana kupinga kitendo cha kijana mmoja kukojolea Quran.
Kwa sasa mabomu ya machozi yanapigwa ili kuwatawanya waandamanaji hao ambao wamezingira kituo cha Polisi wakitaka kijana huyo atolewa la sivyo watakichoma moto kituo hicho.

Mkuu wa Dar Es Salaam,Said Meck Sadick,Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar Es Salaam Suleiman Kova na Sheikh wa Mkoa wa Dar Es Salaa,Alhaj Musa Salum,wamewataka waislam Jijini Dar Es Salaam kuacha Vurugu zisizokuwa na tija kwa kosa lililosababishwa na ubishani wa watoto kuhusu Quran takatifu,jambo ambalo limesabaisha vurugu huko eneo la Chamazi Mbagala ambapo magari yalivunjwa vioo na kuvunjwa kwa makanisa Matatu.

No comments:

Post a Comment