Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, October 26, 2012

WAFANYA BIASHARA WA MADUKA ARUSHA WAWAPIGA WAFANYAKAZI WA MANISPAA ..!

Kampeni ya kuliweka jiji la Arusha katika hali ya usafi imeingia dosari baada ya vurugu kubwa kutokea baina ya wafanyabiashara wa maduka jijini hapa kuwapiga watumishi wa halmashauri ya jiji hadi polisi kuingilia kati kwenye mtaa wa Majengo ya zamani Jijijini hapa leo na maduka kufungwa kwa muda na shughuli kusimama.

Wakiongea na wanahabari baadhi ya mashuhuda wamewaeleza wanahabari kuwa wasimamizi wa usafi walipita kwenye maduka na kuwaambia kuwa waingize bidhaa zao ndani ya maduka hali iliyoleta kutokuelewana kati ya wasimamizi hao na wafanyabiashara kulekopelekea jeshi la polisi kutia timi na hali kuharibika na shughuli kusimama kwa maduka kufungwa.

Wamaeleza kuwa wafanyabiashara hao walichukuliwa na polisi na maduka ya mtaa huo kufungwa kuepusha vurugu hizo na hali ya amani kutoweka kwa muda kwenye maeneo hayo huku waliopewa zabuni ya kutangaza wakipokea kichapo kutoka kwa wafanyabiashara hao na kuzua tafrani kwenye mtaa huo mida ya mchana.

Alipoulizwa na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Liberatus Sabas alisema kuwa yeye hana taarifas kwa kuwa ndio anaingia ofisini baada ya kuwepo kwenye shughuli za kumsindikiza makam wa raisin a kwenda kwenye tukio la kupigwa kwa bomu kwa katibu wa bakwata mkoa wa Arusha Abdul Kareem Jonjo aliyelazwa kwenye hospitali ya Mkoa ya Mount Meru jijini hapa.

Na kuwa atalitolea taarifa pindi atakapoletewa taarifa hizo na kuwa suala hilo teyari lipo kwenye utekelezaji wa sheria na kuwataka wananchi na wakazi wa jiji hili kujenga mazoea ya kufuta sheria bila shuruti kwani kwa yeyote atakayekiuka sheria za nchi hatua kali zitachuliwa dhidi yao na jeshi la polisi litatekeleza wajibu wa kulinda usalaama wa raia na malizao.

Akiongea na wanahabari kaimu mkurugenzi wa jiji la Arusha Omary Mkombole alisema kuwa teyari walikwisha toa elimu sasa sheria inachukuwa mkondo wake na kuwataka wafanyabiashara na wakazi wa jiji hili kwa ujumla kufuata sheria za usafi wa jiji kwani mlipuko wa magonjwa ukitokea ni suala la wote na tujenge mazoea ya kuweka mazingira yetu katika hali ya usafi.

No comments:

Post a Comment