
UMEWAHI
kujiuliza; kwanini mastaa wengi hawadumu na wenzi wao? Nimeamua
kuchambua mada hii kwa sababu tunao mastaa wengi kwenye jamii yetu ambao
wana uhusiano ama na mastaa wenzao au watu wa kawaida.

Pia,
wapo watu ambao wanatarajia kuwa na uhusiano na mastaa, wakati kuna
ambao tayari wapo ndani ya penzi na watu maarufu. Pamoja na hayo yote,
wengi huwa wanashindwa kudumu kwa muda mrefu na mastaa kwa sababu za
hapa na pale.
Katika
mada hii ambayo nimeifanyia utafiti wa muda mrefu, itakufanya mpya
katika uamuzi wako, ndani ya uhusiano na staa au staa ambaye yupo
katika uhusiano na mwenzi asiye staa.
Labda
tuwekane sawa kidogo, hapa namzungumzia mtu maarufu katika jamii,
maarufu kwa maana ya kujulikana sana. Ustaa wa mtu unaweza kusababishwa
na kazi au sanaa. Mathalani, sanaa za maigizo, soka, ndondi, riadha,
siasa, urembo, utangazaji, uandishi wa habari, mitindo, utunzi,
uchoraji, uchongaji, biashara nk.
Siwezi
kutaja moja kwa moja majina ya mastaa, lakini naamini nimeeleweka
vyema kuwa nawazungumzia watu wa aina gani. Watu wanaojulikana sana
katika jamii kulingana na kazi zao za kila siku.
WASIKIE MASTAA
Wakati
naandaa mada hii, nilipata bahati ya kuzungumza na baadhi ya mastaa
ambapo walitoa maoni yao. Kwa bahati mbaya sana, wote niliopata
kuzungumza nao, walipojua mazungumzo yetu yangeishia kuwa mada gazetini
waliomba kuhifadhiwa majina yao.
Hebu
wasikilize: “Kiukweli kaka Shaluwa, naweza kusema sisi wanawake
wenyewe ndiyo wenye matatizo...asikudanganye mtu, ustaa kazi.
Ukishakuwa maarufu, unataka mambo mengi; vipodozi, gari, nguo mpya,
kujirusha, simu iwe na full vocha nk.
“Sasa
kama unakuwa na boy ambaye anajifanya anakuchunga sana, inakuwa ngumu
kudumu na sisi tulivyo jeuri, akikuacha asubuhi, jioni kiwanja
unakutana na mwingine.”
Huyu ni staa wa muziki wa dansi nchini kama alivyozungumza nami jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
“Kiukweli
huwa tunaacha sana mademu, lakini siyo suala la umalaya hapo brother
Shaluwa. Kuna mambo mawili makubwa; kwanza, mwanamke anakuwa anapenda
ustaa wako na siyo penzi la dhati, pili anakubana na kukupangia sana
ratiba...niseme kwamba, wivu unazidi!
“Unajua
unapokuwa msanii, unakuwa na mambo mengi, shoo kibao kila week-end,
safari za mikoani nazo hazina idadi, club ndio usiseme, sasa kwa hali
hiyo, lazima uwe na mwanamke smart kwa kila kitu.
“Tuongee
ukweli, hakuna mtu anayekubali kuwa na mpenzi tapeli, sisi hatuna
matatizo, lakini kama umefuata jina langu au pesa, nitakushtukia soon
na hapo ndipo nitakapompiga kibuti na maisha yanaendelea,” ndivyo mmoja
wa kinara katika Bongo Fleva anavyosema.
Hebu
sikia kauli ya msanii huyu wa filamu: “Wanawake wanapenda umaarufu
wetu, kwahiyo ukiwa naye siku mbili, ukimshtukia unamtema, hapo ndipo
penye tatizo bro. Mimi sihitaji mtu anayependa jina langu, nahitaji
penzi la dhati.”
TATIZO NI NINI?
Kikubwa ni katika KUELEWA na kutofautisha mapenzi na ustaa. Kama
umempenda, umpende kwa mapenzi ya dhati, achana na ustaa wake, lakini
lazima umjue mwenzi wako na uende naye jinsi anavyotaka.
Mapenzi ya kitapeli au kufuata mali na umaarufu hayana nafasi kabisa
katika maisha ya sasa, yote yanawezekana lakini kwa kukubali kujifunza
na kubadilika kulingana na mwenzi wako alivyo.
UPO KWENYE UHUSIANO NA STAA?
Kama nilivyotangulia kusema awali, sina maana kwamba mastaa wote
hawawezi kuishi na wenzi wao bila kuwepo kwa migogoro, ni baadhi yao!
Pamoja na kuwa na migogoro hiyo ambayo mwisho wake mara nyingi imekuwa
ni kuachana, hakumaanishi kwamba, mastaa hawafai kuwa na wapenzi.
Hapa nataka kuzungumza na wale ambao tayari wapo katika uhusiano na
mastaa na wale ambao wanatarajia kuwa na wenzi wenye majina makubwa
kwenye jamii. Hebu pitia vipengele vifuatavyo;
Usiwe na wivu sana!
Ni kweli kwamba, kati ya alama za mapenzi ya dhati ni pamoja na wivu,
lakini unapokuwa na uhusiano na mwenzi staa, lazima upunguze wivu. Hii
haina maana kwamba, umuache awe kicheche, awe na mapatna wengi, hapana!
Mara nyingi mastaa huwa wanaiga mambo ya Kizungu, mathalani husalimiana
kwa kukumbatiana, kuandikiana sms kwa maneno ya mapenzi kama dear,
sweetie, mpenzi n.k, ukikutana na mazingira kama hayo, kuwa mpole,
lakini fanya uchunguzi wako taratibu bila ya yeye kujua. Penye ukweli,
uongo hujitenga.
Kwa Hisani ya GPL
via www.fredynjeje.blogspot.com
No comments:
Post a Comment