Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, October 16, 2012

WAKAZI WA DARAJA MBILI ARUSHA WATAKIWA KUWA MAKINI KATIKA KUCHAGUA VIONGOZI...!

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) mkoani Arusha kimeendelea na mikutano yake ya kampeni katika uchaguzi mdogo wa  kata ya Daraja mbili wilayani Arusha na kuwataka wakazi wa kata hiyo kutochagua vyama vinavyohamasisha vurugu,maandamano na mauaji.

Akihutubia mwishoni mwa wiki iliyopita katika kampeni za uchaguzi huo zilizofanyikan katika uwnaja wa Lamlawa mwenyekiti wa CCM mkoani Arusha,Onesmo Ole Nangole aliwaambia wakazi wa kata hiyo kwamba sifa ya mji wa Arusha imetoweka kutokana na vurugu,maandamano na mauaji kurindima mkoani hapa.

Aliwaambia kwamba Arusha umekuwa ni mji wa maandamano,vurugu na mauaji kana kwamba hauna wakazi wazalendo na kuwataka wakazi wa kata hiyo kuwa makini na vyama vinavyochangia matukio hayo.

“Arusha umekuwa ni mji wa maandamano na vurugu kila kukicha kana kwamba hauna wenyeji sifa ya mji wa Arusha imetoweka sasa kuweni makini na baadhi ya vyama vinavyohamasisha vurugu”alisema Ole Nangole

Hatahivyo,alisema kwa mujibu wa safu mpya ya uongozi wa CCM wilaya na mkoa ambayo imechaguliwa hivi karibuni wana uhakika CCM itashinda uchaguzi huo na nyingine mbalimbali kwa kuwa hakuna mamluki ndani yake.

Alisema kwamba katika uongozi uliopita wa CCM mkoani hapa kulikuwa na mamluki ndani ya chama chao ambapo waligundua mchana watu hao walikuwa CCM na usiku wapinzani hivyo wamewatimua wote ili kukisafisha chama chao.

“Tulikuwa na wana CCM mchana usiku wapinzani lakini tumewatimua wote huu uongozi wa sasa umejipanga kuhakikisha tunashinda chaguzi mbalimbali mkoani Arusha nina na imani na tembeeni vifua mbele wana CCM”alisisitiza Ole Nangole

Naye,mgombea wa udiwani kupitia chama hicho,Phillip Mushi akinadi sera zake aliwaambia wakazi wa kata hiyo wamchague kwa kuwa anatambua kero na mahitaji yao kwa kuwa yeye ni mkazi  wa kata hiyo.

Aliwaambia ya kwamba endapo wakimchagua atashirikiana nao bega kwa bega kutafuta maeneo ya kufanyia biashara hususani  kwa wafanyabishara ndogondogo maarufu kama wamachinga.

Mushi,alisema kwamba  pindi wakimchagua atajitahidi kukarabati shule za sekondari  na msingi za daraja mbili  ili kuzifanya kuwa za kisasa huku akihaidi kumalizia ujenzi wa zahanati ya kata hiyo ambayo imekwama  hadi sasa.

Naye,diwani wa kata ya Terat,Julius Ole Sekeyan alitumia muda wake jukwaani kumshambulia aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini kwamba ndiye aliyehusika kuwahamasisha wamachinga kuvamia eneo la kiwanja cha Ermoil hivi karibuni  na kulaani tukio hilo kwamba  ipo siku Lema atashawishi watu kuvamia makazi ya watu.

No comments:

Post a Comment