Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, October 16, 2012

WAKAZI WA KILIMANJARO WAJITOKEZA KUTOA MAONI YA KATIBA MPYA...!

Watumishi wa serikali, vyama vya siasa na mashirika mbali mbali mkoani Kilimanjaro, jana wamejitokeza kutoa maoni yao mbele ya wajumbe wa tume ya kukusanya na kuratibu maoni ya katiba inayoendeleza na zoezi hilo mkoani Kilimanjaro.

Zoezi hilo limefanyika katika ukumbi wa mikutano kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, ambapo watumishi na vingozi hao wametoa maoni ambayo kwa asilimia kubwa yamegusia madaraka ya rais, muungano na tume ya uchaguzi.

Wakichangia kwa nyakati tofauti wadau hao wamesisitiza rais kupunguziwa madaraka, umuhimu wa kuwa na tume huru ya uchaguzi, katiba kuruhusu mgombea binafsi, uwepo wa mahakama ya kadhi na umuhimu wa
kuwa na serikali tatu.

Zoezi la kukusanya maoni kwa mkoa wa Kilimanjaro, limeendeshwa na wajumbe wa tume hiyo wakiongozwa na Profesa Mwesiga Baregu, ambapo kesho wanaendelea na zoezi hilo litakalohitimishwa Novemba 6, mwaka huu kwa mkoa wa Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment