Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, October 6, 2012

WAUGUZI MIREMBE WAGOMA WAKIDAI POSHO

Wauguzi  wa Hospitali ya Mirembe mkoani hapa wamegoma kufanyakazi kwa madai ya kutaka kuongezewa posho ya muda wa ziada wa kazi.

Wauguzi hao wanadai kwamba kiwango cha fedha wanacholipwa cha Sh. 3,000 ni kidogo ikilinganishwa na kile wanacholipwa wengine.

NIPASHE ilipotembelea hospitalini hapo jana asubuhi ilifanikiwa kuwaona baadhi ya wagonjwa wakiwa na ndugu zao huku wakirandaranda hospitalini hapo wakiwa na mafaili yao.

Mmoja wa wauguzi hospitalini hapo ambaye hakutana jina lake litajwe aliliambia NIPASHE kwamba wameamua kugoma baada ya kuona serikali haiangalii umuhimu wao.

“ Julai wauguzi tulilipwa kiasi cha Sh. 10,000 lakini mwezi uliofuatia tulishangaa kuona tunapewa malipo tofauti jambo ambalo lilitushtua na tukataka kujua sababu zake,” alisema.

Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Erasmus Mndeme alikanusha kuwepo kwa mgomo wa madaktari na kuongeza kuwa waliogoma ni wauguzi.

Aidha, alisema kuna baadhi ya madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo wanaingia kazini mara mbili kwa siku na hilo linatokana na kuwepo kwa uhaba wa wafanyakazi.

Dk. Mndeme alisema suala la malipo katika Hospitali hiyo lipo kwenye viwango tofauti kulingana na vyeo vya watumishi.
“Kuna watumishi wanaolipwa Sh. 25,000, 20,000, 15,000, 10,000  na kiwango cha chini cha malipo ni Sh. 5000 hadi 3,000.

“Kulingana na viwango hivyo ndiyo maana wauguzi wanaona wanapunjwa bila kufahamu kuwa katika nafasi walizonazo kuna utofauti mkubwa wa malipo wanayotakiwa kulipwa pindi wanapofanya kwenye ziada ya masaa,” alisema.

No comments:

Post a Comment