Watu wawili wamekufa papohapo na
wengine wawili wamejeruhiwa vibaya katika ajali ya lori lililokuwa
likitokea jijini Dar es Salaam kwenda Muheza mkoani Tanga.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa 3 usiku katika maeneo ya Msata, mkoani Pwani.
Akizungumzia tukio hilo ndugu wa karibu marehemu, Yustino Mnyela alisema kuwa sababu ya ajali hiyo ni lori kukatika usukani na kumshinda dereva na kupinduka mara tatu.
Aliwataja waliokufa kuwa ni Geofrey Aloyce Majuto na Scola Denis Daimoni, wote wakazi wa Kwabada wilayani Muheza na maiti zimehifadhiwa katika hospitali ya Tumbi, Kibaha.
Alisema kuwa watu waliyojeruhiwa ni dereva wa lori hilo, Doni Luka na mtoto ambaye jina lake halijafahamika mara moja na wamelazwa katika hospitali ya Tumbi Kibaha.
Polisi imethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwaonya madereva kwenda mwendo kasi.

No comments:
Post a Comment