Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, December 12, 2012

HII HAPA ALBUM YA KALA JEREMIAH YENYE NYIMBO 23 INAYOKWENDA KWA JINA LA PASAKA...!


Hii hapa album mpya ya Kala Jeremiah aliye kuwa mshiriki katika Bongo Star Search na sasa amekamilisha Album yake na hili hapa chini ndio cover la album yake na pia ameandika ujumbe mzito kwa mashabiki wake kuhusiana na album yake. 

HABARI ZA SAHIZI WADAU, HUU NDIO MFANO WA COVER LA ALBUM YA PASAKA YENYE NYIMBO 23 JINA LA PASAKA LIMETOKANA NA WIMBO AMBAO UKO HUMO NDANI AMBAO UNAITWA PASAKA
AMBAO KI UKWELI NI BONGE LA WIMBO. UBUNIFU ULIOTUMIKA KATIKA KUUTENGENEZA WIMBO WA PASAKA NI UBUNIFU WA HALI YA JUU SANA KWA MARA YA KWANZA DUNIANI UTASIKIA WIMBO AMBAO NI MOVIE YA KUTISHA. YANI WIMBO WA DAKIKA 4 NA SEKUNDE KADHAA LAKINI UTAKUWA UMEKUFANYA KUONA MOVIE YA KUTISHA YA MASAA MA WILI NA NUSU. UPANDE WA NYUMA WA COVER HILI HAUTAKUWA HIVYO KAMA ULIVYO HAPO BALI UTAKUWA NAMAJINA YA NYIMBO NA MAJINA YA WASANII WALIOSHIRIKISHWA PAMOJA NA MA PRODUCER WOOTE WALIOSHIRIKI IKIWA NI PAMOJA NA STUDIO ZOTE NILIZOFANYA KAZI YA ALBUM HII. LAKINI PIA JUU YA CD YENYEWE KUTAKUWA NA PICHA NA MAANDISHI. ALBUM INATARAJIWA KUWA SOKONI KUANZIA TAREHE20 MWEZI HUU NA ITAKUWA INAUZWA 5000 ZA KITANZANIA. ITAPATIKANA PIA MIKOANI NA TUTATANGAZA MAENEO HUSIKA ITAKAPOKUWA IKIPATIKANA. OMBI. UKIFANIKIWA KUNUNUA ALBUM HII TAFADHALI USIMWAZIME JIRANI AU RAFIKI KWA KUWA KWA KUFANYA HIVYO UTAKUWA UMEZOROTESHA HARAKATI.PIA KUITUNZA ALBUM HII NI SWALA LA MSINGI SANA KUTOKANA NA NYIMBO ZILIZOMO HUMO SIO NYIMBO ZA KUPITWA NA WAKATI KWA HIYO UKIITUNZA WATAKUJA KUSIKILIZA HATA WAJUKUU ZAKO NA WATAFURAHIA UJUMBE. COVER LA NYUMA LINA NAMBA ZA SIMU NAMBA HIZO NDO ZITAKAZOTUMIKA KUPIGA SIMU KWA AJILI YA MANUNUZI NA TAARIFA ZINGINE MUHIMU. ASANTENI.

No comments:

Post a Comment