Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, December 20, 2012

KINYANG'ANYIRO CHA KUMPATA MCHEZAJI BORA WA SOKA AFRIKA KUFIKIWA LEO...!

Wachezaji wanaowania uzo ya mchezaji bora Afrika, 
(Yaya Toure, Didier Drogba na Alexandre Song)

Na Sabina Chrispine Nabigambo
Shirikisho la soka barabi Africa CAF leo litamtangaza mchezaji bora wa soka kwa mwaka 2012 na hafla ya tuzo hiyo itafanyika mjini Accra Ghana, huku mashabiki wengi wa soka wakimtaja mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Cote d'Ivoire Didier Drogba kushinda tuzo hiyo.


Wengine wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na Yaya Toure naye akitokea timu ya taifa ya Cote d'Ivoire na Alexandre Song wa Cameroon.

Wakati huo huo rais wa shirikisho la soka nchini Cote d'Ivoire Jacques Anouma jana Jumatano aliwasilisha malalamiko yake kwenye mahakama ya michezo mjini Lausanne dhidi ya uamuzi wa CAF mnamo Disemab 10 kukataa ombi lake la kugombea nafasi ya rais wa CAF kwa kigezo kuwa mgombea yeyote anatakiwa kuwa mwanachama wa kamati ya utendaji ya CAF.

Jacques amesema kuwa dai hilo ni njama ya kutaka kumfungulia njia Issa Hayatou Issa kuwa mgombea pekee wa mwaka ujao.

Chanzo: http://www.kiswahili.rfi.fr

No comments:

Post a Comment