Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, December 21, 2012

WAMACHINGA MJINI WALETA KIZAZAA NA KUFUNGA BARABARA...!
MACHINGA wa Mji wa Moshi leo walileta kizaa zaa katika mji wa Moshi baada ya Wafanya biashara hao wadogo kufunga barabara ya Ghala, wakipinga kitendo cha Uongozi wa Manispaa ya Moshi, kuvunja Gereji ya Bantu, wanayoitumia kama sehemu ya kuhifadhia bidhaa zao.

Father Kidevu Blog, ambayo ipo mjini Moshi kwa Shughuli Maalum, ilifika katika eneo la tukio na kushuhudia barabara ya Ghala, ikiwa imefungwa na mabanzi, mawe, Mabati, mananasi, mikate na magari kushindwa kuvuka huku jeshi la polisi la mkoa wa Kilimanjaro, likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Kilimanjaro (RCO), Ramadhan Ng’anzi walikuwepo eneo la tukio kuweka mambo sawa.

Akizungumza na Machinga hao katika juhudi ya kuhakikisha usalama unarejea kama kawaida, RCO Nga’azi aliwataka viongozi wa Wamachinga kuwatuliza wafuasi wao, nakuangalia njia nyingine ya kutafuta haki kwa amani.

Alisema kuna umuhimu wa kila mwananchi kutambua wajibu wa kudumisha amani na kuwakumbusha umuhimu wa kuhakikisha haki wanayoitafuta haikiuki haki za binadamu na Raia wengine wa nchi hii.

Akizungumza na wamachinga hao, muda mfupi baada ya kuwasili katika eneo la tukio, Mkuu wa wilaya ya Moshi, Dkt. Ibrahimu Msengi, aliwaahidi wachinga hao kufanyia kazi tatizo lao na kuwaomba wateue wawaklishi wao wanne ambao aliandamana nao hadi katika ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Bernadeta Kinabo, kuzungumza Tatizo na kulipatia ufumbuzi.

“Nimesikia tatizo lenu na kilio chenu ndio maana niko hapa, nataka niwahakikishie kwamba le oleo mtapata majibu kutoka kwangu, kwa sasa ninachowaomba nim kila mtu arejee katika shughuli zake za kawaida ili amani ya mji wetu uendele kuwepo,” alisema Msengi.

Kwa upande wao, baadhi ya Machinga wanaodaiwa kuvunjiwa na kuharibiwa mali zao katika tukio hilo lililotokea jana , majira ya saa saba usiku, Abdallah Abushehe na Mwamedi Ally, walisema kuwa, asubuhi ya leo waliamka na kufika katika gereji hiyo wanayo itumia kuhifadhia bidhaa zao na kukuta eneo hilo limevunjwa na baadhi ya mali zao kupotea.


“Mimi ni fundi viatu, kawaida yetu ni kuhifadhi bidhaa zetu hapa gereji, wamevunja usiku usiku hata taarifa hawajatupa, hawa wagambo wamezidi kutuonea sana, kila siku wanatukimbiza wanatunyima raha kweli ya kufanya kazi, sasa hivi mkokoteniwangu na magunia yangu ya viatu siyaoni, kwa kweli sisi tumechoshwa na uongozi wa Manispaa,” alisema Ally.


Naye mmiliki wa Gereji ya Bantu lililovunjwa na kuzaa mzozo huo, Abdillahi Ally, alikiri kupata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa mji wa Moshi, Bernadetta Kinabo kuhusu eneo hilo kuwepo katika ramani za ujenzi wa Nyumba za shirika a Nyumba Taifa (NHC).

Alisema kuwa aliwahi kupata Barua kutoka kwa Meneja wa NHC, iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, ikimtaka kuachia sehemu hiyo ndani ya siku mbili, lakini kutokana na kutoridhika na maamuzi ya hayo alifungua kesi Mahakamani. 

No comments:

Post a Comment