Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, December 11, 2012

KUNDI HARAMU LA "LAMBALAMBA" LASAKWA VIKALI NA POLISI...!


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 10/12/2012

Polisi Mkoa wa Dodoma tumeendelea kufuatilia watu wanaoendesha shughuli za “lambalamba” katika maeneo mbalimbali hususani katika wilaya za Chamwino, Kongwa na Mpwapwa. Watu hao wanaojifanya kufichua wachawi, uchunguzi wetu umebaini kuwa wanatapeli watu kwa ajili ya kujipatia fedha.

Pili shughuli wanazoendesha ni kinyume cha sheria za nchi na ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binanadamu za kuwaita baadhi ya watu kuwa ni wachawi kwa lengo la kujipatia fedha.

Vitu wanavyojifanya kuvitoa ndani ya nyumba au maduka ya watu, tumegundua wao wenyewe hutumia baadhi ya watu kwenda kuviweka / kuvipandikiza na baadaye wanapokuja hujifanya wamevikuta kwenye nyumba ya mtu anayetuhumiwa kuwa ni mchawi. 

Wananchi waelewe kuwa wanatapeliwa fedha zao na hao watu waliobuni mradi wa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwani wamejionea wanachangishwa fedha kabla ya kuwaita na hata wanaodaiwa kuwa wachawi, hudaiwa kiasi cha fedha.

Inasemekana kwamba wanaoendesha shughuli za lambalamba wanadai pia kutafutiwa wanawake wa kulala nao jambo ambalo ni hatari kwani mali ya kwamba ni kinyume cha sheria na unyanyasaji wa kijinsia na pia upo uwezekano mkubwa wa kuambukizwa magonjwa ikiwepo UKIMWI. 

Katika kulifanyia kazi tatizo hilo tarehe 09/12/2012 tumefanikiwa kuwakamatwa watu wane (4) waliokuwa wanajiandaa kuendesha shughuli za lambalamba katika kijiji cha Vilundilo Wilayani Kongwa. Watu hao ni:-

  1. MKOMBOZI S/O SALEHE
  2. HADIJA D/O TUPA
  3. JOYCE D/O NHEMBELO
  4. SIWEMA D/O KWAELI

Wanawake hao walikuwa ni kwa ajili ya kuwapikia lambalamba hao.
Upelelezi unakamilishwa ili wafikishwe mahakamani wakati wowote. Ufuatiliaji wa lambalamba wengine waliokimbia unaendelea pamoja na viongozi wanaoshirikiana nao.

Pia Polisi Mkoani Dodoma inamshikilia kwa mahojiano IDDI S/O RAMADHANI PANDAUYAGA @ NGOSHA, MSUKUMA, Mkazi wa DODOMA MAKULU baada ya kulalamikiwa na wananchi wengi kwa kujipatia fedha kwa njia udanganyifu kuwa anawauzia viwanja. Hadi sasa ameshatapeli zaidi ya Tshs. 24,537,000/= kuanzia mwezi Agosti, 2012. Huwarubuni watu kuwa viwanja hivyo ametumwa na wafanyakazi wa CDA kuviuza.

Wito kwa wananchi wasikubali kurubuniwa kuwa wanauziwa kiwanja na kutoa fedha bila kuthibitisha kiwanja hicho kama kipo na ni halali.

[D. A. MISIME – ACP]
KAMANDA WA POLISI [M] DODOMA

No comments:

Post a Comment