Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, December 11, 2012

Maadhimisho Ya Siku Ya Haki Za Binadamu Duniani Na Miaka 64 Ya Tamko La Kimataifa La Haki Za Binadamu...!

 




Na: Rodrick Maro
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na mashirika mengine, yamefanikiwa kufanya maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani, miaka 64 ya Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu, la mwaka 1948 na Kilele cha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Jinsia.

Mambo mbalimbali yalifanyika, ikiwa ni pamoja na maandamano, mawasilisho ya hotuba mbalimbali na burudani kutoka kwa vikundi mbalimbali vikiwemo Jakaya Arts Theatre, Dancers wa Kibasila Secondary, Maigizo Human Rights Clubs kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu (UDSM, IFM, Tumaini, Mwl. Nyerere) na kasha mjadala wa pamoja, uliojikita zaidi kwenye uadilifu na hatma ya taifa letu.

Mgeni rasmi katika siku hii alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa LHRC, Askofu Mstaafu Elinaza E. Sendoro (aliyewakilishwa na Wakili Fransic Stolla - Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika), wawakilishi wa Umoja wa Ulaya, Mkurugenzi Mtendaji wa WiLDAF mama Judith Odunga, Mkurugenzi Mtendaji wa WLAC, na wawakilishi kutoka mashirika mbalimbali na wanaharakati toka pande mbalimbali za Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment