Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, January 6, 2013

ANYWA NA SUMU NA KUFARIKI DUNIA KWA KUKOSA ADA YA SHULE...!

Mtu mmoja amefariki dunia jijini Dar es Salaam kwa kunywa sumu.

Akithibisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo, alisema marehemu aliyetambuliwa kwa jina la Gift Mbaga (23) alifikishwa Hospitali ya Temeke, Januari 4, 2013 kwa matibabu.

Kamanda Kiondo alisema ilibainika wakati wa kupatiwa matibabu kuwa Mbaga alikuwa amekunywa sumu nyingi.

“Chanzo cha kifo hicho inasadikiwa marehemu alikunywa sumu kwa madai ya ugumu wa maisha, alikosa ada ya kuendelea na masomo baada ya kumaliza kidato cha sita katika Shule ya Junior Seminary, iliyopo mkoani Morogoro. Baada ya kunywa sumu hiyo marehemu alikuwa anatokwa na mapovu mengi mdomoni, ambapo baada ya kufikwa na mauti hayo mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke, huku tukiendelea na uchunguzi zaidi,” alisema RPC Kiondo.


Chanzo: www.wavuti.com

No comments:

Post a Comment