Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, January 24, 2013

HAYA NDIO MAANDALIZI YA FILAMU YA GHOST OF MY MOM..!

      KIKUNDI cha sanaa cha Choper Art's Group chenye makazi yake Moshi, Mkoani Kilimanjaro leo kimeanza Maandalizi rasmi ya kutengeneza Filamu yao mpya itakayofahamika kwa jina la "GHOST OF MY MOM". Filamu hiyo yenye mandhari ya kiafrika inayolenga maisha halisi ya kiafrika.

Akizungumza na King Jofa Mkurugenzi wa Choper Art's Group ndugu George Choppa alisema, Maandalizi ya awali ya filamu hiyo yamekwisha kamilika na sasa wasanii wanajiandaa kwa ajili ya kuanza kuchukua video za filamu hiyo Ambayo inatarajiwa kuanza baada ya wiki moja kuanzia sasa. Ambapo filamu hiyo inatarajiwa kutengenezwa na kampuni ya UWEZO PRODUCTION ya jijini Dar es Salaam chini ya mtaalamu wake Fareed Uwezo.

Mkurugenzi huyo aliwataja baadhi ya wadau walioweza kujitoa na kuhakikisha ndoto za vijana wenye vipaji katika sanaa ya filamu walio katika kikundi cha Choper Art's Group ni Pamoja na kampuni ya GRM INVESTMENT chini ya mkurugenzi wake mkuu anayefahamika kwa jina la Dada ROSE huku akitoa shukrani za dhati kwake kwa kujitolea kuwa mlezi na mshauri wa kikundi cha Choper Art's Group. 

Choppa aliweza kupeleka shukrani zake kwa Ngorika Bus Service kwa kuweza kuonesha moyo wa uzalendo kwa kutoa mchango wa fedha itakayosaidia katika utengenezaji wa filamu hiyo. Pia alimaliza kwa kutoa wito kwa wadau mbalimbali kuweza kujitokeza kusaidia vikundi mbalimbali vya vijana wenye uhitaji wa kukamilisha ndoto zao kupitia sanaa wanayoifanya.

Baadhi ya wasanii na Wadau wa Filamu Moshi, Wakiwa na Mkurugenzi wa Choper Art's Group, Aliyesimama mstari wa nyuma kavaa shati jeupe.

Wasanii wa Choper Art's Group wakiwa katika pozi baada ya Mazoezi, Hapo ni Pipiro a.k.a M-Pesa aliyevaa tisheti nyeupe na Noor aliyevaa tisheti nyekundu.

No comments:

Post a Comment