Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, February 12, 2013

JACKLINE WOLPA AELEZEA SIRI NYINGINE ZA MAISHA YAKE KAMA ASINGEKUA STAR WA BONGO MOVIE...!

MSANII wa filamu Tanzania Jackline Wolpa anaamini mafanikio hutokana na juhudi, kujituma pamoja na kutimiza malengo yako uliyojiwekea kwa kipindi ulichokusudia

Msanii huyo wa filamu alielezea maisha yake yako nje ya Tasnia ya filamu alipokutana na mwandishi wa safu hii

Wolpa mbali na kuigiza pia yeye ni mcheza netiboli katika timu ya bongo movi akiwa anachukua nafasi ya mfungaji 'GS' huku akiwa tishio kwa timu pinzania kwa uwezo alionao na jinsi anavyoweza kutumia urefu aliokuwa nao kwa kufunga magoli mengi

Alianza kucheza netiboli akiwa shuleni na huko ndipo alipopata ujuzi wa mchezo huo ambapo mpaka sasa ameweza kuwa tishio kwa kuumudu mchezo huo na kuweza kuisababishia ushindi kwa timu anayoichezea

Alisema kuwa anapata muda wa kutosha kufanya mazoezi kila siku jioni na asubuhi hivyo mazoezi yanamsaidia kujenga mwili wake pia na kumpa pumzi zinazomsaidia kucheza kipindi chote bila ya kupumzika mpaka mwisho wa mchezo

Aliendelea kusema kuwa kwa upande wake anathamini sana mazoezi kwani yanamfanya kuzidi kuwa imara na pia hutumia mazoezi kwake ni kama dawa ya kuondoa uchovu katika mwili wake

Wolpa aliweka wazi kuwa kama ingekuwa si muigizaji basi angekuwa mchezaji mzuri wa netiboli na angeongeza nguvu katika hilo na kuweza kuchezea timu kubwa na anaamini kuwa angefanya vizuri kwenye upande huo

Anaeleza kuwa hatoweza kusahau siku alipoumia vidole vya mikono kwenye mechi iliyokuwa inachezwa katika viwanja vya Leaders Club na aliweza kuendelea kucheza mchezo huo na hatimaye waliibuka washindi katika mechi ya kujipima

Mbali na kucheza netiboli pia msanii huyo ni bingwa wa kuogelea, huku akidai kuwa muda wake mwingi wa mapumziko anautumia kuogelea ili kuweka mwili wake imara

Aliongezea kuwa mara nyingi huwa anaratiba ya nini afanye muda gani na kipi kifanyike wakati gani hiyo ndiyo moja ya kitu anachoamini kuwa kinampa mafanikio makubwa katika maisha yake

Wolpa alisema huwa hapendi kuwa na makundi ya watu hivyo hawezi kuamua kwenda kukaa bar kama hana kazi ya kufanya kwa sababu ratiba yake inakuwa imejaa muda wote ule

Wolpa ambaye pia alikuwa anafanya biashara ingawa sasa anajipanga kuianzisha tena biashara yake ili maisha yake yaendelee kuwa yenye mafanikio kwa juhudu anazozifanya

Aliongezea kuwa anapenda kusoma vitabu muda wa mapumziko zaidi kuliko kwenda kukaa bar na marafiki ambao kwake anahisi laba hawana mafanikio ingawa si kila rafiki ni mwema au ni mbaya hivyo kwa upeo wa kiubinadamu huwezi kutambua hilo kwa haraka

Anasema kuwa kusoma vitabu kunamsaidia kumjenga kiuwezo na fikira pia inamuongezea kuwa mbunifu hususani katika kazi zake za sanaa

Wolpa ni msanii wa filamu ambapo alianza kuigiza mwaka 2009 na filamu iliyomtambulisha ni Amazangu amazao kwa sasa anatamba na filamu nyingi ikiwemo ya Ndoa yangu aliyoigiza na marehemu Steven Kanumba

No comments:

Post a Comment