Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, February 13, 2013

MOTO UMEWAKA TFF WAZIRI AINGILIA KATI, ATUMA UJUMBE MZITO KWA TENGA ...!

Siku moja baada ya kamati ya rufaa ya shirikisho la soka nchini kumuengua mgombea uraisi wa TFF, Ndugu Jamaly Malinzi kutoka kwenye kugombea uraisi katika uchaguzi ujao wa TFF, leo hii wadau tofauti wa michezo wametoa maoni yao kuhusiana na sakata. Mmoja wa wadau aliyepaza sauti kuzungumzia suala hilo ni naibu wa waziri wa michezo, Bwana Amos Makalla.

Akizungumza na Ibrahimu Masoud kupitia kipindi cha michezo cha Sports Extra cha Clouds FM leo usiku, Makalla alisema ameshangazwa sana na kitendo cha kamati ya rufaa kumuengua Malinzi kwa sababu ambazo ameziita hazina mashiko na zimekuosa ushawishi.


"Mimi kama mdau wa soka na michezo kwa ujumla napenda kusema kuhusu hili bila kupepesa macho kwamba kamati hii imepotoka kwenye suala hili. Hii kamati kwenye hili inataka kujishushua heshima, unajua wakati mwingine unaweza kujishushia heshima kwa gharama nyepesi. 


"Sababu walizotoa kumuengua Malinzi zimekosa ushawishi. Hoja walizotoa mimi kama mwanamichezo naona hazina mashiko. Malinzi anakosa vipi uzoefu sasa hivi, huku akiwa kiongozi wa chama cha soka cha mkoa? Alishawahi kuwa katibu wa klabu kubwa kama Yanga kwa miaka kadhaa, pia hi huyu huyu Malinzi ambaye aligombea uraisi wa TFF dhidi ya Tenga wakati huo, sasa iweje kipindi hicho aweze kugombea na sasa hivi ashindwe eti kisa kakosa uzoefu. Uzoefu gani wanauzungumzia ambao alikuwa nao kipindi hicho na asiwe nao sasa," aliongeza Naibu waziri huyo.


"Maamuzi ya namna hii yanadhoofisha kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya Jakaya Kikwete katika kurudisha uzalendo kwenye michezo. Raisi amefanya mengi katika kuhamasisha watu kupenda michezo, sasa hivi watanzania tumeanza kupenda michezo. Tenga ameongoza vizuri na sasa tunahitaji TFF makini itakayokuwa ikiongozwa na viongozi makini watakaoiongoza soka yetu na hatimaye tuweze kwenda AFCON na World Cup.


"Mimi kama waziri wa Michezo ninamuomba Raisi Tenga aliyewateua watu wa kamati hiyo aingilie suala na kuweka sawa, hali isije kuwa mbaya na watu wakaanza kupoteza upenzi na soka kwa mambo ya ajabu kama haya. Viongozi wa kamati kama walitaka tujue na madaraka na uwezo wa kufanya hili walilofanya wamefanikiwa kwa hilo, lakini sasa nawaomba watumie busara. Wasiwafanye watanzania waache kupenda mpira, wasiturudishe nyuma na jitihada za serikali katika kukuza michezo. Nawaomba wamrudishe Malinzi kura zipigwe kwa haki tupate uongozi bora." - alimaliza naibu waziri huyo wa michezo na utamaduni.

No comments:

Post a Comment