Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, April 25, 2013

GODBLESS LEMA ASAKWA NA POLISI KILA KONA,GARI LAKE HILI HAPA LIKIBEBWA NA POLISI...!

 
Kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha kililazimika kutumia Mabomu ya Machozi kuwatuliza wanafunzi waliokuwa wakishinikiza kuandamana baada ya mwanafunzi mwenzao kuuawa kwa kuchomwa kisu na watu wasiojulikana majira ya saa nne usiku wa kuamkia leo.  

 Tukio hilo liliamsha hisia za wanafunzi hao na kuwafanya wakusanyike kuelekea kwa mkuu wa mkoa wa Arusha kwa madai kwamba matatizo yao huwa hayafikishwi ipasavyo, hivyo wanataka kuyawasilisha wenyewe.   

Juhudi za uongozi wa chuo kuwatuliza wanafunzi hao zilishindikana, na ilipofika majira ya saa nne asubuhi, Mbunge wa jimbo la Arusha alifika katika eneo hilo kuwasikiliza wanafunzi hao. 

"Tunatoa dakika thelathini mkuu wa mkoa awe ameshafika hapa, kama hajafika ndani ya muda huo, tunaandamana wote, mimi mbele nyie nyuma mpaka ofisini kwake" alisema 

Mheshimiwa Lema.Baada ya mkuu wa mkoa kufika eneo la tukio aligoma kuzungumza na wanafunzi hao, akidai kwamba hawezi kuongea mpaka Mh.Lema aondoke, ndipo atapanda kuzungumza na pia alilalamika kwamba hamna kipaza sauti kwa hiyo hawez kupaza sauti yake kuzungumza na watu wasio na nidhamu. 
 
Maneno hayo yalipandisha hasira ya wanafunzi hao lakini walitulizwa, na kipaza sauti kikaandaliwa katika ukumbi wa chuo maaruf kama "main cafetaria" ili mkuu huyo azungumze.
Wanafunzi walikusanyika eneo hilo kumsikiliza lakini alivyoanza kuongea, wanafunzi walisikika wakimzomea kwa madai kwamba ameonesha dharau.  

Wanafunzi walianza kuzomea na kumrushia chupa zaa maji na mawe  mkuu wa mkoa na hapo ndipo ilibidi mabomu ya machozi yatumike kuwatuliza wanafunzi wa chuo hicho. 

Kwa muda wa masaa mawili imekuwa ikisikika milio ya mabomu chuoni hapo mpaka hali ilipo tulia kabisa. 

Kwa sasa hali ni shwari chuoni hapo ila polisi wametapakaa huku na kule wakisema wanamtafuta Mbunge wa jimbo la Arusha kwa madai kuwa ndiye anaye chochea mgomo huo wa wanafunzi. 

Mbunge huyo alikimbia kuelekea kusikojulikana na kutelekeza gari yake chuoni hapo, ambayo polisi walilazimika kuivuta kwa "breakdown" car kuelekea kituo cha polisi. kama inavyoonekana katika picha.
Gari ya Mh.Godbless Lema ikiochukuliwa na polisi kutoka eneo la tukio
Polisi wakichukua gari ya mbunge wa jimbo la Arusha.
Source: sangafesto

No comments:

Post a Comment