Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, April 22, 2013

KIGODA AKIRI UMEME NI KIKWAZO KIKUBWA CHA MAENDELEO TANZANIA...!

Waziri wa  Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda  alisema kuwa  moja ya changamoto nchini ambayo inarudisha maendeleo nyuma  hasa ya viwandani ni tatizo la kutokuwapo kwa umeme  wa uhakika.   
Akizungumza  jana Dar es Salaam katika uzinduzi wa Kiwanda cha  Kutengeneza Juisi cha Wabantu kilichopo mkoani Tanga, Kigoda alisema kuwa Serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa  nishati ya umeme inakuwa ya uhakika ili kufikia lengo. 
Kigoda alisema kuwa ili kuweza kufikia lengo  kwa kiwanda hicho kipya, lazima nishati ya kueleweka na itakayowezesha ufanisi kwa haraka  iwapo kwani mitambo inayotumika  ni ya kisasa hivyo ni Serikali lazima itilie mkazo suala zima la umeme.
“Ni matumaini yangu mna malengo ya kufika mbali,lakini nijuavyo mimi umeme katika viwanda ni changamoto kubwa, hivyo tutahakikisha Serikali inatilia mkazo hasa kwenye nishati ya umeme ili muweze kufika  panapostahili,” alisema Kigoda.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Kiwanda hicho, Zahor Rashid  alisema kuwa  lengo la kuanzisha kiwanda hicho ni kukuza pato la taifa kwa kutengeneza juisi nzuri yenye kiwango ambayo itauzwa mikoa yote nchini, baadaye  Afrika Mashariki hatimaye kuvuka mipaka hadi kupata soko la Afrika kwa ujumla,
Alieleza kuwa kiwanda hicho kimeanzishwa mkoani Tanga kwa sababu ndipo kwenye matunda mengi ya kila aina hivyo ni rahisi kupata matunda  yenye kiwango na kwamba kiwanda hicho  kitakuwa na vituo kila mkoa wenye matunda  kwa wingi ili kuendelea kutengeneza juisi nzuri zaidi
“Tutajitahidi kuweka kituo kila mkoa unazalisha matunda kwa wingi ili kuhakikisha  tunayatumia  ipasavyo  badala ya kuyaacha yaharibike,” alisema Rashidi.
 
Habari na  Magreth Munisi,
Chanzo - Mwananchi

No comments:

Post a Comment