Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, April 26, 2013

MZEE WA MIAKA 49 AMLAWITI MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO MWENYE ULEMAVU WA AKILI...!

MKAZI mmoja wa Kitasha Mengeni wilayani Rombo aliyefahamika kwa jina la Balthazar Pankras Swai mwenye umri wa miaka 49 anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wa darasa la tano mwenye ulemavu wa akili. Na taarifa kutoka katika jeshi la polisi zinadhibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku wa kuamkia tarehe  25 Aprili 2013 katika kijiji cha Aleni Chini.

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limesema kitendo hicho cha kikatili alichofanyiwa
mwanafunzi huyo wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mengeni wilayani Rombo, kimemsababishia mtoto huyo maumivi makali katika sehemu zake siri. Mbinu iliyotumika kumkamata mzee huyo ni polisi wakishirikiana na polisi jamii wa kijiji hicho kwa usimamizi wa Mwenyekiti Correntini Masawe.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema mtuhumiwa pia ni mhalifu sugu kwani alishawahi kufungwa gerezani miaka ya nyuma kutokana na matukio ya kihalifu  huku wakilaani kitendo alichokifanya mtuhumiwa na kuvitaka vyombo vya dola kuchukua mkondo wake.

No comments:

Post a Comment