Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, April 26, 2013

PICHA NA MAELEZO YA MAADHIMISHO YA MIAKA 49 YA MUUNGANO UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ...!

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama lililoandaliwa maalum kwa ajili maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa na Mabalozi pamoja na wageni waalikwa mbalimbali ili kushuhudia maadhimisho hayo.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-UWANJA WA UHURU)

4
Rais Wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kulia akiwa na viongozi wengine katika jukwaa kuu kutoka kushoto ni Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Idd, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

7
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akiingia uwanjani katika gari maalum huku akisindikizwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.


Vikosi vilivyo pita na kutoa heshima mbele, kikosi cha Ulinzi JWTZ, kikosi cha  Jeshi la Ulinzi JWTZ, Kikosi cha Jeshi la Kujenga taifa JKT na Kikosi Maalum Cha Bendera kikitoa heshima zake bele ya Rais Jakaya Kikwete.

17
Watoto wa halaiki wakionyesha ujumbe mbalimbali kuhusu Muungano wetu mbele ya Rais Jakaya Kikwete na maelfu ya Watanzania waliohudhuria katika maadhimisho hayo.

No comments:

Post a Comment