Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, April 8, 2013

VIDEO YA WIMBO WA JAILUN UITWAO STAR ALIOMSHIRIKISHA DIAMOND YAKAMILIKA....!


Msanii wa Muziki wa kizazi kipya anayekuja kwa kasi Tanzania JAILUN anayetamba katika vituo vingi vya Radio na TV na wimbo wake unaokwenda kwa jina la ANAKUIBIA aliomshirikisha NEIBA anatarajia kuachia Video ya Wimbo wake Mpya Unaokwenda kwa Jina la STAR aliomshirikisha NASEEB ABDUL aka DIAMOND.

Akipiga Story na Shushushu wa Kingjofa Jailun amesema Video hiyo itakua moto wa kuotea mbali kwa kuwa huko ndani wameepotezana kuanzia mavazi mpaka style za kucheza. Akizungumzia Wimbo huo   alio mshirikisha Diamond amesema ilikuwa vigumu kumpata Diamond na kuweza kufanya nae kazi lakini alisema Diamond ni mtu mwelewa na pia wametoka mbali wameweza kufanya show Boma na pale Moshi mkoani Kilimanjaro. Jailun yupo na wenzake Rich Mavocco,Timbulo,Sam Waukweli na Dayna kwa meneja wao Papaa Misifa huku yeye akiwa chini ya mameneja wawili ambao ni Papaa Misifa na Man Ngereza.
Jailun akimzungumzia NGEREZA amesema Ngereza ni meneja wake ambae wametoka mbali tangu kipindi Jailun akiwa anaishi Boma Wilaya ya Hai lakini yeye ni mzaliwa wa Arusha na kwa sasa yupo Dar es salaam akifanya kazi ya muziki.
Alizidi kufunguka kuhusiana na Meneja wake huyo Jailun amesema kuwa Ngereza aliweza kusababisha yeye kurekodi wimbo wa Nalia na wewe ambao aliufanya kwa Mazuu pale Mazuu Records.
Akizungumzia kuhusu Muziki  Amesema Muziki uko kwenye damu na anahitaji sapoti kutoka kwa wadau ili aweza kuutangaza vema mziki wa Tanzania na amesisitiza kuwa muziki sio uhuni bali ni kazi kama kazi zilivyo kazi nyingine.

Haya sasa mwenye macho na atazame Jailun huyooo anakuja kwenye kichupa……!

No comments:

Post a Comment