Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, April 18, 2013

WABUNGE WATANO WA CHADEMA WASIMAMISHWA KUINGIA BUNGENI..!

Mh. Tundu Lissu Mbunge wa Jimbo la Singida Vijijini na Mwanasheria wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.

Naibu Spika Ndugai jana  aliamuru Tundu Lissu atolewe nje ya Bunge huku wabunge wa upinzani wakizomea na kusema hatoki mtu. 
Amri hiyo ilitokea baada ya yeye  kuingilia kati mchango wa Mh. Mwigulu Nchemba aliyesema kwamba udini ni jambo geni hapa nchini.
 Tanzania imeongozwa na CCM tangu uhuru, na maraisi wote wamekuwa wakitoka CCM, raisi wa kwanza alikuwa mkristo, wa pili muislam, wa tatu mkristo na wa nne ni muislam, akasema kama udini ni jambo geni watanzania tujiulize limekujaje? Kwanini sasa na sio wakati huo?

Akasema katika kampeni za uraisi 2010 Dr. Slaa akiwa katika kampeni mkoani Singida alitumia viongozi wa dini kufanya vikao vya kampeni badala ya kutumia wanachama wa chama chake na viongozi hao wapo tayari kutoa ushahidi.
Ndipo Tundu Lissu aliposimama na kuomba mwongozo, spika akamwambia atulie kwa sababu Susan Kiwanga tayari amepewa nafasi akalisemea hilo na muda ni mdogo Lissu akang'ang'ania ndipo Naibu Spika akaamuru askari amtoe nje Lissu.

Pamoja na hayo Naibu spika amewafungia vikao vitano kinyume na kanuni za Bunge Mh. Lema, Mh. Mbilinyi. Mh. Kiwia, Mh. Msigwa, Mh. Wenje.

No comments:

Post a Comment