Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, May 4, 2013

AFYA YA NOORBAZIR WA CHOPPER GROUP INAENDELEA VIZURI KWA SASA...!

 Noorbawazir akiwa hospital KCMC baada ya kufanyiwa upasuaji
 
SALMA Musa maarufu kama Noorbawazir ni msanii chipukizi wa maigizo ambaye katika Filamu ya "GHOST OF MY MOM" iliyochezwa na Chopper Group alicheza kama Tabu mtoto wa bibi Msiza ambaye mzimu wa mama yake ulimuingilia na akabadilika na kuwa chozi muuaji, filamu hii nzuri na ya kuvutia imeshakamilika na siku si nyingi itaingia sokoni. Noorbawazir pia ni muhasibu katika kikundi maarufu cha maigizo kinachofahamika kwa jina la Chopper Group chenye makazi yake mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Noorbawazir kwa sasa anasumbuliwa na kidole tumbo (Appendex) ambapo alianza kupata matibabu katika kituo cha afya cha pasua tokea jumanne ya tarehe 30 April 2013 ambapo alikaa katika kituo hicho cha afya mpaka jana asubui tarehe 3 April 2013 alihamishiwa katika hospital ya rufaa ya KCMC iliyopo mjini Moshi ambapo jana hiyohiyo usiku saa mbili alifanyiwa upasuaji, ila kwa sasa anaendelea vizuri. Na anaonesha kuwa na matumaini makubwa sana ya kurejea katika hali yake ya kawaia na kuendelea kuwakonga mashabiki wake kama kawaida.


  Noorbawazir akiwa na mama yake mzazi katika hospital ya rufaa ya KCMC.


Noorbawazir akipewa pole na King Jofa akiwa katika hospital ya rufaa ya KCMC.

Mtandao huu wa www.kingjofa.blogspot.com unampa pole sana Noorbawazir na kumuombea apone mapema na kurejea katika hali yake ya kawaida.

No comments:

Post a Comment