Leo nipo na Mohamed Waziri maarufu kama DJ Virus
ni maarufu sana ukanda wa kaskazini mwa Tanzania hususani katika mkoa Kilimanjaro kiukweli
ni DJ mwenye umri mdogo lakini ana uwezo mkubwa sana katika kufanya kazi ya u’DJ kazi ambayo
inahitaji umakini wa hali ya juu. DJ Virus alianza kufanya kazi ya u’DJ kwenye
club ndogo ndogo za mjini Moshi miaka ya 2007 wakati akiwa shule ya secondary na
hakupenda kuishia hapo maana alikua na imani kubwa sana na kazi hii ambayo aliiipenda
na pia aliahidi kuitendea haki kazi hii ya u’DJ kwa kuwa aliamini ni kazi ambayo
inaweza kumletea mafanikio makubwa katika maisha yake.
DJ Virus kwa sasa ni DJ katika radio inayofaamika kama Kibo
Fm iliyopo wilaya ya Hai - mjini Moshi pia anafanya kwenye baadhi ya Club na
kwenye matamasha mbalimbali amekua akifanya kazi hiyo na anasema kwa mtu yeyote
akimuhitaji kwa ajili ya kufanya show sehemu yoyote yeye yupo tayari kikubwa ni
kuwasiliana na uongozi wa Kibo Fm na kuweka utaratibu mzuri ambao hautaweza
kuadhiri ratiba zake wala ratiba za ofisini (Kibo Fm). Baada ya kunielezea
hayoyote sikupenda kuishia hapo bali nilitamani pia kufahamu mambo mengi
hususani yanayogusa tasnia ya burudani na wadau wa burudani pia.
Nilimuuliza ni nyimbo za aina gani ambazo ukizipiga unahisi
kama watu wengi sana
wanazipenda na kuzifurahia? “actually dj kama dj
anatakiwa apige nyimbo zote kwani watu wanaosikiliza ngoma ni wengi sana kila mtu anatamani kusikia ladha yake ila kiukweli ki
bongo bongo watu wanapenda sana
bongo flavour” Alijibu DJ Virus
Kwa hapa mkoa wa Kilimanjaro unahisi kama
producers, wasanii na watangazaji au maDJs mnaushirikiano mzuri kwenye
kufanikisha harakati za muziki? “Hapa mkoani banaaa
kiukweli ma dj ma presenter na ma producer hawana ushirikiano kila mtu anataka
kuwa zaidi ya mwenzake hatuwezi kufika kwa staili hii alafu ma dj wengi wana
copy na ku paste hakuna tofauti ya ladha” Alijibu DJ Virus
Wewe kama DJ unadhani kati ya producer na msanii ni yupi
anailikupewa lawama endapo nyimbo itakua mbaya? “inategemea
coz producer ndo anamsikia msanii kwa mara ya kwanza hivyo yeye ndo anajuwa
kuwa msanii yupo vizuri au bado kama bado anapaswa kumrudisha nyumbani akafanye
mazoezi tena ya sauti au vitu vingine lakini sasa ivi ma producer nao wapo
after money wao hawaangalii tena hivyo vitu bali wao sasaivi wannaangalia
mkwanja tu so nyimbo ikiwa mbaya wa kwanza kulaumiwa ni producer” Alijibu DJ Virus
Wewe kama DJ ni juhudi gani binafsi ambazo unazifanya
kufanikisha mziki hususani kwa mziki unaofanywa na wasanii wanaotokea mkoa wa
Kilimanjaro? “mimi kama mimi nawapa airtime ya kutosha
ngoma wanazonipa nazitendea haki sana kiukweli na kuna baadhi ya matamasha
makubwa yanatokea pia nawapaga nafasi ya upaform jukwaani ili wazidi kujulikana
na pia wanapewa kipato kidogo kama kupewa big up kwa alichokifanya jukwaani” Alijibu DJ Virus
Kuna lawama kwamba nyie ma DJ wa radio za hapa mkoani
Kilimanjaro huwa hamzipi airtime ya kutosha ngoma za wasanii wa nyumbani
(Kilimanjaro) mpaka wasanii wawape hela? “Hahahaaaaaa amna
bana ila kiukweli mi sijawahi kupokea hela ya msanii ila wapo baadhi ya wasanii
pia walishawahi kuniambia kuwa walishawahi kwenda katika moja ya radio hapa
moshi naihifadhi kwa jina jamaaa walitakiwa watoe elfu 20 ili ngoma yao ichezwe radioni na
pia wakitaka kufanya interview watoe hela kidogo pia” Alijibu DJ Virus
Huyo alikye hitaji hela anaitwa nani na anafanya kwenye
radio gain? Maana ni vyema watu wakamfahamu hususanni wasanii wa mkoa wa
Kilimanjaro ili wakiwa na ngoma mpya watafute na 20,000 ili ngoma yao isikike radioni? “hapana nimesema hivyo ili kuondoa misunderstanding” Alijibu DJ Virus
Huoni kwa kuto kumtaja utakua unakumbatia maovu ambayo
mwisho wa siku yatazidi kuudididmiza mziki wa vijana wa mkoa wa Kilimanjaro? “Kwa kweli siwezi kumtaja ila wakisikia au wakuisoma
habari hii wale wasanii na yule DJ atawza kujirekebisha tabia yake” Alijibu DJ Virus
Nasikia pia nyie ma
DJ huwa mkipewa CD na wasanii wadogo mnatabia ya kuwaambia kuwa “MBONA CD IPO
EMPTY?” Na msanii anapojaribu kukuelewesha kuwa CD sio Empty huwa mnazidi
kusisitiza kuwa CD ni Empty kumbe maana ya CD EMPTY ni kwamba CD HAINA HELA ili
ngoma yako ikapate airtime.
Nashukuru sana
kwa time yako ila wafikishie salamu ma DJ wote wenye tabia za kudai hela ili
wazipe airtime ngoma za wasanii wachanga siao fresh bana, maana wanawakatisha tama
na mwisho wa siku pia ma DJ nao wanaharibu vipindi vyao kwa kuacha kucheza
ngoma nzuri za wasanii wachanga na kung’ang’ania kucheza ngoma mbaya kwa kuwa
zimelipiwa hela..
Bovya kwenye mshale hapo chini usikiliza Mixing iliyofanywa na DJ Virus
No comments:
Post a Comment