Mbunge wa
Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, amelishutumu Jeshi la Polisi
mkoani Arusha kwamba limekwa kipeperushi cha Mkuu wa Mkoa wa huo, Magesa
Mulongo, kutokana na kutumika katika kumsafisha katika sakata la
kutumiwa ujumbe wa vitisho katika simu yake ya mkononi. Lema
ametoa kauli hiyo jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari
kufafanua taarifa ya jeshi hilo kwamba ujumbe mfupi wa vitisho
aliotumiwa haukutumwa kutoka katika simu ya Mulongo.
“Nimesikitishwa
sana na taarifa zilizotolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha,
Liberatus Sabas, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Mei 5, mwaka
huu kuhusu ujumbe niliotumiwa sasa inathibitisha bila mashaka kuwa Jeshi
la Polisi Arusha, hasa Mkuu wake anatumika,” alisema Lema.
Alisema kuwa ujumbe huo alioupokea ulikuwa unasomeka “Umeruka kihunzi
cha kwanza nitakuonyesha kuwa mimi ni Serikali , ulikojificha
nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi”.
Lema alisema amekuwa akijiuliza maswali mengi yanayokosa majibu, kuhusu
taarifa ya Jeshi la Polisi na mtandao wa simu kampuni moja (jina
tunalihifadhi), amabyo ni pamoja na kwa nini jeshi hilo lilikataa
kuchukua maelezo yake, juu ya tuhuma hizo nzito dhidi ya Mkuu wa Mkoa
ambaye amemtumia meseji kupitia simu yake ya mkononi kama
alivyolalamika.
Alisema ni takribani mwezi mmoja umepita tangu atoe malalamiko yake
Polisi, lakini Jeshi hilo limeona ni busara kwenda kampuni hiyo ili
kutafuta mawasiliano yake Mulongo.
Wiki iliyopita, Sabas alisema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa
simu iliyotumika kumtumia Lema ujumbe wa vuitisho ni ya kampuni ya nje
ya nchi na siyo namba ya Mulongo.
“Nilipokuwa rumande msaidizi wa Mkuu wa Makosa ya Upelelezi Arusha
alinifuata na kuniomba nimpe simu yangu, nilimwambia sina nimemwachia
mke wangu, na walimtafuta mke wangu na kumuomba hiyo simu na
kumhakikishia kuwa akiwapa simu wataniachia na kunifutia kesi.
Mke wangu aliwajibu kuwa simu aliidondosha kwenye gari ya Polisi ile
ambayo walinichukua nayo usiku wa siku waliyonikamata,” alisema Lema na
kuongeza.
SOURCE: NIPASHE
No comments:
Post a Comment