Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, June 12, 2013

CHOPER ART’S GROUP WASHIKANA UCHAWIKundi la sanaa la Filamu mkoa kilimanjaro Choper Art’s Group leo limekutana pamoja katika mkutano wao mkuu wa Mwaka ambao ulikuana agenda mbalimbali ikiwemo viongozi kutoa mapato na matumizi ya kikundi katika muda wa utengenezaji wa Film yao ya Mom’s Ghost ambayo wametengeneza mwezi  wa pili mwaka huu.

MWENYEKITI WA CHOPA ART'S GROUP AKIMTULIZA MMOJA WA VIONGOZI WA KUNDI HILO.

Wakati Mwenyekiti wa kikundi hicho aitwaye George Migire akitoa mapato na matumizi ya kikundi hicho uliibuka mzozo mkubwa wa matumizi ya kiasi cha shilingi elfu sitini tu. Haapo ndipo mambo mengi yalipoibuka baada ya siri kubwa kuibuliwa kuwa kiongozi mmoja wa kikundi hicho kutumia fedha hizo kwa kwenda mganga kwa ajili ya kukinga kundi hilo.

 HUYU NDIYE KIONGOZI ANAYETUHUMIWA KUTUMIA
 PESA KWENDA KWA MGANGA

King Jofa akizungumza na Kiongozi huyo anayesadikiwa kutumia fedha hizo kwa ajili ya kwenda kwa Mganga kuhusiana na tuhuma hizo alipinga vikali na kusema alitumia fedha hizo kwa ajili ya mambo ya ndani ya kikundi na alirudisha stakabadhi kwa muhasibu wa kikundi.
Haya sasa mambo ndio hayo kumbe makundi yanaendaga kwa waganga ili wawe juuu.  

No comments:

Post a Comment