Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, June 22, 2013

KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977 SEHEMU YA TATU HAKI NA WAJIBU MUHIMU

Haki ya Usawa Usawa wa binadamu
Sheria ya 1984 Na.15 ib.6
12.-(1) Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni
sawa.
(2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na
kuthaminiwa utu wake.
Usawa mbele
ya Sheria ya
1984 Na.15 ib.6
13.-(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na
wanayo haki,
bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki
sawa mbele ya
sheria.
Sheria ya Na.4
ya 1992 ib.8
Sheria ya 2000
Na.3 ib.5
(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na
mamlaka
yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti
lolote ambalo
ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.
(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na
jumuiya ya
watu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na
vyombo
vinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na
sheria au kwa mujibu wa sheria.
(6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya
sheria,
Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au
zinazozingatia
misingi kwamba -
(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji
kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo
kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa
na
haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na
pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya
kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au
chombo hicho kingenecho kinachohusika;
(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la
jinai
kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka
itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa
hilo;
(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya
kitendo chohote ambacho alipokitenda hakikuwa ni
kosa chini ya sheria, na pia kwamba ni marufuku
kwa
adhabu kutolewa ambayo ni kubwa kuliko adhabu
iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendwa;
(d) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa
binadamu,
heshima ya mtu itatunzwa katika shughuli zote
zinazohusu upelelezi na uendeshaji wa mambo ya
jinai na katika shughuli nyinginezo ambazo mtu
anakuwa chini ya ulinzi bila uhuru, au katika
kuhakikisha utekelezaji wa adhabu;
(e) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa
kinyama
au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.
Haki ya Kuishi
Haki ya kuwa hai Sheria ya 1984 Na.15 ib.6
14. Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka
kwa jamii
hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria.
Haki ya Uhuru wa mtu binafsi Sheria ya 1984 Na.15
ib.6
15.-(1) Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi
kama
mtu huru.
(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa
huru na
kuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu
yeyote
kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa
kizuizini,
kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru
wake
vinginevyo, isipokuwa tu-
(a) katika hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa na
sheria, au
(b) katika kutekeleza hukumu, amri au adhabu
iliyotolewa na mahakama kutokana na mtu kutiwa
hatiani kwa kosa la jinai.

No comments:

Post a Comment